Na, Rashid Mkwinda, Mbeya
WATU saba wamefariki dunia na wengine 41 kujeruhiwa vibaya baada ya Lori aina ya Fuso lenye namba za usajili T855 ACJ kugongwa kwa nyuma na lori aina ya SCANIA lenye namba za usajili T 463 na kupinduka korongoni katika mlima wa Iwambi kuelekea Mbalizi mkoani Mbeya.
Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema kuwa lori aina ya Fuso lilibeba watu waliokuwa wakitokea mazishini ambalo lilikuwa mbele ya SCANIA lililokuwa katika mwendo wa kasi hivyo dereva wa gari hilo alishindwa kulimudu ndipo tela la gari lake lilipoligongalori na kusababisha kuanguka korongoni.
Mmoja wa majeruhi aliyelazwa katika wodi namba moja ambaye ana mauimivu ya kifua na mkono aliyejitambulisha kwa jina la Hassan Ahmad alisema kuwa wao walikuwa wakitokea mazikoni ndipo Lori lenye tela lilipowagonga kwa nyuma na wao kutupwa korongoni.
Waliokufa katika ajali hiyo wametambuliwa kwa jina moja moja kuwa ni Boni mkazi wa Mbalizi,Rabi au (Jaymo) mkazi wa Mbali na mtoto mdogo anayekadiriwa kuwa na umri wamiaka mitatu aliyefahamika kwa jinala Angel Brighton.Kwa mujibu wa muuguzi wa zamu katika kitengo cha msaada wa haraka Bi. Anna Nyenye ni kwamba jumla ya majeruhi walioletwa hospitalini hapo ni 41 ambapo kati yao 14 waliruhusiwa baada ya kupatiwa matibabu.
Muuguzi mkuu wa hospitali ya Rufaa Dkt. Thomas Isidory aliwataja baadhi ya majeruhi waliolazwa kuwa ni Bw.Regani Kazumba,Bw. Goden Mwaminya, Enesia Duyange,Siana Moses, Vumi Mwakipesile, Ilunga Lusaja, Kethy Simbeye,Grace Simyonga na mmoja aliyefahamikakwa jina la Ikupa.Wengine ni Elizabethy Mwalingo,Godfrey Sako,Michael Charles,Josephina Ebby, Kissa Josephat, Hassan Hamad,Mariamu Mwakipesile, Juliethy Kabote, Josina Kyando, Vumilia Edward, Bupe Bahati,Bertha Kanyiko, Halima Samson, Emmy Omar, Quine Wilson na HabibaGwaza na Nuru Datsun.
Alisema kuwa kati ya majeruhi hao 14 wameruhusiwa baada ya kupatiwa matibabu na kwamba waliolazwa baadhi yao hali zao zinaendelea vizuri na wengine ambao wamelazwa katika wodi namba moja, mbili na tatu.Wakati huo huoAbiria waliokuwa wakisafiri katika Basi la Upendo linalofanya safari zake kati ya Mbeya na Dar es salaam lenye namba za usajili T 191 AHM wamenusurika kifo baada ya Basi hilo kupinduka katika eneo la Chimala wilayani Mbarali janaasubuhi.
Mashuhuda wa ajali hiyo walisema dereva wa Basi alikuwa akimkwepa mwendesha baiskeli ndipo mbele yake akakutana na Lori la Kampuni ya Dhandoo ambalo lilimkwangua kwa pembeni na kuangukia upande wa dereva.
Majeruhi ambao ni abiria waliokuwa wakisafiri katika basi hilo wamelazwa katika hospitali ya misheni ya Chimala.
No comments:
Post a Comment