hii ni inshu ambayo imemtokea mshaji wangu hivi karibuni pale maeneo ya Ubungo kwenye mataa,maana aletewa simu inayofanana hivihivi na hii akitakiwa kuinunua wa kiasi cha shilingi za kibongo 50,000,na yeye alipoona hivyo si ndio akaona huu ubwete ngoja niilipie fasta fasta kabla wanga hawajaonana,kidume akazama mfukoni fasta na kumlipa huyo jamaa huku na yeye akiipokea simu na kuiweka mfukoni bila kuichunguza huku akiamini kuwa amewini kwa siku hiyo kwani kapata simu bomba kwa bei ya ubwete.alipofika mbele ya safari yake si ndio akataka aichunguze fresh na aweke laini yake kwa ajili ya kuanza kujidai nayo,hapo ndipo alipotaka kurudisha namba kwa saa godi kwa kile alichokiona katika simu aliyonunua kwani hivi mnavyoona hapo ndivyo alivyoviona na yeye.hivi kama ungekuwa ni wewe ungefanya nini mara baada ya kuona mambo ambayo hukuyategemea?halafu inakuwa vipi kama mkwanja wenyewe haukuwa wako yaani labda liambiwa uupeleke sehemu??
Tuesday, April 28, 2009

Home
Unlabelled
ushawahi kukumbana na kanyaboya hii??
ushawahi kukumbana na kanyaboya hii??
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Hapo ubungo mataa ndo kawaida yao kuuza simu feki.. Kuna mshkaji tulikuwa naye kwenye gari siku moja wakamuonyesha simu (waliitoa kwenye bahasha), wakaifungua kabisa,akaona betri na kila kitu! Muuza simu akaanzia 40,000 mshkaji akashuka naye hadi 10,000! Taa zikawaka, mshkaji akachukua simu, muuzaji akapewa hiyo buku 10 tukaendelea na safari. Kufika mbele akataka atoe simu yake aanze kujidai, hamadi akakuta sabuni ya kipande! Sijui alibadilishaje bwana! Jamaa noma kweli wale! Halafu hawakosi wateja hadi leo!
ReplyDelete