Kinyang`anyiro cha kumtafuta mrembo wa Tanzania Ulaya mwaka huu,”Miss Tanzania Europe 2009` kinatarajiwa kufanyika Juni 27 kwenye ukumbi wa Silverspoon ulipo pembeni ya uwanja maarufu wa Wembley,uliopo kaskazini mwa jiji la London.
Akizungumza Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya shindano hilo, Juma Mabakila alisema kuwa wamepata baraka zote kutoka kwenye kamati ya Miss Tanzania kwa kupewa idhini ya kuandaa shindano hilo la Ulaya.
Awali miaka miwili mfululizo onyesho hilo lililikuwa mahsusi kwa ajili ya warembo wa London pekee, lakini kamati ya Miss Tanzania mwaka huu imetoa kibali cha kuandaa mashindano ya Ulaya kutokana na kufanikiwa katika shindano la Miss London.
“Kweli tulifanikiwa katika mashindano yetu tuliyofanya miaka miwili iliyopita, tulipeleka washindi wetu kushiriki katika mashndano ya Miss Tanzania na wote walifanikiwa kuingia katika kumi bora, mwaka huu tumejiandaa va kutoksha, “ alisema Mabakila..
Mabakila alisema kama ilivyo katika mashindano yaliyopita, pamoja na kutangaza utamaduni wa Tanzania, kubwa zaidi ni kutumia sanaa ya urembo kutangaza vivutio vya utalii..
Awali mwaka jana Big Brother Afrika wa mwaka juzi Richard Bezuidenhout ambae ni Mtanzania alikuwa mmoja wa majaji wa shindano hilo, huku akisaidiwa na mwenyekiti wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga na Jacqueliney Mafuru.
Wasanii wanaotarajiwa kutumbuiza katika onesho hilo ni Banana Zoro na Hafsa Kizinje(pichani ),wasanii wa Kiganda wenye makazi yao hapa London na kujijengea jumaarufu mkubwa, Da Twinz..
Taji la Miss Tanzania UK mwaka 2008, Tusekile Mwakibinga wakati mwaka 2007 mshindi alikuwa, Gladness Katega.Warembo wawili wa Miss Europe 2009 wanakwenda moja kwa moja kushiriki shindano la Miss Tanzania.
No comments:
Post a Comment