Rais Jakaya Kikwete ameteua Wakuu wa Wilaya 15 , 7 wamestaafishwa na 54 wamehamishwa vituo, ili kuongeza chachu ya uwajibikaji katika kusimamia na kuratibu mipango mbalimbali ya maendeleo na uchumi ili kutimiza malengo ya serikali.
Kwa mujibu wa taarifa toka Ofisi ya Waziri Mkuu, Ma-DC wawili wamepangiwa kazi zingine na wawili wengine wamepangwa kufanya kazi katika jumuiya za chama tawala - CCM.
Walioteuliwa kwa mara ya kwanza ni Ms Mercy Sila (Arumeru - Arusha), Mr Norman Sigalla (Hai – Kilimanjaro), Col Issa Njiku (Misenyi - Kagera), Ms Angelina Mabula (Karagwe - Kagera), Dr Rehema Nchimbi (Newala - Mtwara), Francis Isaac (Mbulu - Manyara), Lt Col Benedict K Kitenga (Rorya - Mara) na Lt Col Cosmas Kayombo (Mbarali - Mbeya).
Wengine ni Christopher Ryoba Kangoye (Kwimba - Mwanza), Queen Mashinga Mulozi (Ukerewe - Mwanza), Fatuma Mwassa (Mvomero - Morogo), Fatma Ally (Nanyumbu - Mtwara), Juma Solomon Madaha (Tunduru - Ruvuma), Anatory Choya (Kishapu - Shinyanga) na Erasto Sima (Korogwe - Tanga).
Ma-DC waliostaafu ni Elias Marugu (Misenyi - Kagera), Deusdedit Mtambalike (Muleba - Kagera), David Holela (Babati - Manyara), Hawa Ngulume (Mbarali - Mbeya), Mashiba H Mashiba (Kyela - Mbeya), Col Peter Madaha (Nyamagana - Mwanza) na Gilbert Dololo (Kibaha - Pwani).
Ma-DC waliopangiwa kazi zingine ni Patrick Tsere aliyekuwa DC (Ilala – Dar es Salaam), na Doreen Kisamo (Uyui - Tabora). Mr Martin Shigela ambaye alikuwa DC (Lindi - Lindi) sasa ni Katibu Mkuu wa UVCCM ambapo Husna Mwilima (Hai - Kilimanjaro) sasa ni Katibu Mkuu wa UWT.
Waliobadilishwa vituo ni pamoja na Elias W. Lali kutoka Arusha – Arumeru kwenda Ngorongoro, Evans Balama toka Arusha – Arusha kwenda Ilala, Jowiko W Kasunga kutoka Arusha – Ngorongoro kwenda Monduli, Col Fabian I Massawe toka Dar es Salaam – Kinondoni kwenda Muleba, Abdallah A Kihato toka Dar es Salaam –Temeke kwenda Kyela.
Wengine ni Zainab Kwikwega toka Dodoma – Bahi kwenda Kasulu, Dr Ian J. Langiboli toka Dodoma – Chamwino kwenda Babati, Capt Seif A. Mpembenwe toka Dodoma – Kondoa kwenda Handeni, Halima Dendego toka Dodoma – Mpwapwa kwenda Kilosa, Lephy B Gembe toka Iringa – Makete hadi Chamwino na Elaston J. Mbwilo toka Iringa – Iringa kwenda Mtwara.
Wengine ni Darry I Rwegasira toka Iringa – Njombe kwenda Mpwapwa, Said M Mkumbo toka Kagera – Chato kwenda Temeke, Frank A Uhahula toka Kagera – Karagwe kwenda Tarime, Lt Col John Mzurikwao toka Kigoma – Kibondo kwenda Mpanda, Saidi Bwanamdogo toka Kigoma – Kasulu kwenda Kondoa, Raymond H Mushi toka Kilimanjaro – Rombo kwenda Arusha.
Wengine ni Jordan Rugimbana toka Kilimanjaro – Mwanga hadi Kinondoni, Rashid M Ndaile toka Lindi – Nachingwea kwenda Chunya, Anna Magowa toka Lindi – Liwale kwenda Hanang, Elias Goroi toka Manyara – Mbulu kwenda Nachingwea, Capt Geoffrey Ngatuni toka Manyara – Hanang kwenda Musoma.
Walohamishwa wengine ni Saveli Maketta toka Mara – Musoma hadi Namtumbo, Stanley Kolimba toka Mara – Tarime kwenda Uyui, Ms Miriam L Lugaila toka Mbeya – Rungwe hadi Misungwi, Halima Kihemba toka Mbeya – Mbozi kwenda Kibaha, Fatuma L Kimario toka Mbeya – Chunya kwenda Igunga.
Wengine ni Athuman H Mdoe toka Morogoro – Kilosa kwenda Mwanga, Hawa Ng’humbi toka Morogoro – Mvomero hadi Makete, Gishuli M Charles toka Mtwara – Mtwara kwenda Njombe, Jackson W Msome kutoka Mtwara – Newala kwenda Rungwe, Capt Assary Geofrey Msangi toka Mtwara – Nanyumbu kwenda Iringa.
Wengine ni Samwel Kamote toka Mwanza – Ilemela hadi Bukoba, Danhi Makanga toka Mwanza – Kwimba kwenda Kibondo, Magalula S Magalula toka Mwanza – Misungwi hadi Lindi, Paul Chiwile toka Mwanza – Ukerewe kwenda Liwale, Mathew K Nasei toka Mwanza – Magu kwenda Muheza, Lt Col Serenge M. Mrengo kutoka Pwani – Bagamoyo hadi Ilemela, Ali N Rufunga toka Pwani – Rufiji kwenda Manyoni.
Wengine ni Major Bahati Matala toka Rukwa – Sumbawanga kwenda Kahama, Thobias Mazanzala toka Rukwa – Mpanda kwenda Sumbawanga, Gabriel Kimolo toka Ruvuma – Namtumbo kwenda Mbozi, Peter Toima Kiroya toka Ruvuma – Tunduru kwenda Rombo, Amina Masenza toka Ruvuma – Mbinga kwenda Shinyanga.
Waliohamishwa vituo wengine ni Khadija R R Nyembo toka Shinyanga – Kishapu kwenda Chato, Col (rtd) Edmund Mjengwa toka Shinyanga – Shinyanga kwenda Mbinga, Magesa Mulongo toka Shinyanga – Bukombe kwenda Bagamoyo, Florence A Horombe toka Singida – Singida kwenda Bukombe, Pascal Mabiti toka Singida – Manyoni kwenda Singida, Cleophas Rugarabamu toka Tabora – Igunga kwenda Nyamagana.
Wengine ni Kassim Majaliwa Majaliwa toka Tabora – Urambo kwenda Rufiji, Lt Winfrid F Ligubi toka Tanga – Handeni kwenda Urambo, Elizabeth Mkwasa toka Tanga – Korogwe kwenda Bahi na Zainab Kondo toka Tanga – Muheza kwenda Magu.
No comments:
Post a Comment