HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 19, 2009

Dr.Mwakyembe Aongea Na Wanahabari

[caption id="attachment_2832" align="aligncenter" width="450" caption="Dk. Harrison Mwakyembe akiongea na waandishi "] Dk. Harrison Mwakyembe akiongea na waandishi [/caption]

Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, amekiri kuanzisha Kampuni yaumeme wa upepo ya Power Pool East Afrika Ltd, kutokana na anachokiitagharama zitokanazo na mitambo ya kukodi.


Amesema mkataba wa serikali na Kampuni ya Independent Power TanzaniaLimited (IPTL) wa miaka 20 ni mzigo mzito kwa serikali na taifa kwaujumla, kwa kuwa unataka Tanesco ndiyo inunue mafuta ya dizeli, vipurina gharama za mashine.


Akizungumza na waandishi wa habari, Mwakyembealisema pamoja na hilo, bado Serikali ya Tanzania inatakiwa pia kuilipa IPTL Sh bilioni 3.7 kwa mwezi ambayo ni sawa na Sh milioni103.7 kwa siku.


“Jamani huu ni mzigo mzito kwa Watanzania tena kuubeba kwa miaka 20,ndipo kwa uchungu tuliona na tukaamua tufikirie njia mbadala yakuwaondolea Watanzania mzigo huu,” alisema.


Alisema waliamua kuanzisha kampuni hiyo, mwaka 2004 baada ya kuchapishwa kitabu cha UglyMalaysian ambacho kilikuwa kinausema vibaya mkataba wa Tanesco na IPTL hasa suala la gharama za uendeshaji mitambo.


Miongoni mwa washirika wengine wa Mwakyembe katika kampuni hiyo ni Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa, ambaye ni Mjumbe wa Bodi yaWakurugenzi wa Tanesco.


Wengine ni Emmanuel Kasyanju, Prosper Tesha,TBC (1998) Limited, Isaac Mwamango, Mwacha Kagoswe, Josephine Pinana Athumani Ngwilizi, MECCO Limited ya Maungo Kwabibi, BestonMwakalinga, Niels Dahlmann na Leonard Tenende.


Dk. Mwakyembe alisema IPTL ilinunua mitambo yake kwa dola milioni 120za Marekani lakini kutokana na fedha nyingi ilizokuwa ikilipwa kwasiku, baada ya miezi minne inaweza kununua mitambo mingine kama hiyo.“Huu ni unyonyaji hatuwezi kuuvumilia.”


Alisema kwa upande wa Dowans,hali ni tofauti kwa kuwa hakuna hata mkataba, mitambo yake ni mibovu tofauti na ya IPTL, imeishitaki Tanesco, inadaiwa na benki nyingi naTanesco wenyewe wanadaiwa.


“Sasa jamani utanunua kitu chenye matatizo?”


Alisema kampuni nyingineza umeme zimekuwa zikiila nchi kupitia mtindo huo akitolea mfano waAggreko ambayo inalipwa Sh milioni 62, APR Mwanza Sh milioni 76, Dowans Sh milioni 158 na Songas ambayo bado inalipwa Sh milioni 265 zote ni kwa siku.


Alisema akiwa na wenzake wengi wakiwamo maprofesa, wahandisi naviongozi wengine wa siasa, waliamua kutafuta suluhu la tatizo hilo kwa kuanza mchakato wa kuanzisha kampuni ya umeme wa upepo ambayo inatarajiwa kuzalisha megawati 1,800.


Alisema kwa kuwa bado kampuni hiyo iko kwenye mchakato na haijaanza kuzalisha, hawezi kuelezea maslahi yake juu ya kampuni hiyo na kwamba kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati Teule kuchunguza Richmond na kuzungumzia suala la ununuzi wa mitambo ya Dowans, havina uhusiano wakimaslahi na kampuni hiyo ya umeme wa upepo.


Alisema kwa sasa wanahitaji mitambo na Sh nusu trilioni, ili wawezekuanza kuzalisha umeme.


“Kampuni hii ni ya watu masikini hawana fedhani ndoto kuzipata hizo nusu trilioni lakini tunajitahidi, hivyo siweziku-declare interest (kueleza uhusiano wangu) ni sawa na mkeo akiwa namimba uanze kutangaza kuwa mtoto wako atakuwa daktari.


”Aliwataka Watanzania kuelewa kuwa maslahi ya nchi yao yatazingatiwa naWatanzania wenyewe na ndiyo maana wao wako katika mapambano, kwanikilichotokea ni moja ya mapambano na hawataacha kupambana.


Akijibuswali juu ya yeye akiwa kiongozi kujihusisha na biashara, alisemaiwapo mradi huo utaanza kuzalisha umeme, atachagua aende wapi, kwenyeubunge au kuwa mfanyabiashara.


“Lakini naamini kuwa ubunge si kazi ya kudumu japo kwa upande wangusina ukomo na kazi hii, ila ifahamike kuwa sina mkataba na Bunge.


”Kuhusu madai yaliyoandikwa na chombo kimoja cha habari kuwa ameumbuka,alisema hawezi, hana sababu na wala hatarajii kuumbuka, hasa kutokanana ukweli kuwa tuhuma hizo zimetolewa na chombo cha habari cha Mbungewa Igunga, Rostam Aziz.


Hata hivyo, Rostam naye alidai kuwa yeye si mwandishi wa habari hivyo kama Mwakyembe anatuhumiwa kwenye vyombo vyake vya habari, anatakiwa ajibu hoja na si kumtafuta au kumwandama mtu.


Akizungumza na waandishiwa habari leo Dar es Salaam, Mwakyembe alisema imezuka tabia ya baadhiya viongozi waliochafuliwa katika jamii, kutumia vyombo kujisafisha, lakini kwa mtindo wa kuwachafua wengine.


Alisema kwa wanaomtuhumu kwa kutetea ununuzi wa mitambo ya IPTL nakumshangaa anapogomea ununuzi wa mitambo ya Dowans, wafahamu kuwakampuni hizo mbili hazifanani wala mazingira yake hayahusiani. “Nikama usiku na mchana.”


Dk. Mwakyembe alisema IPTL ilikuwa na mkatabana Tanesco tangu Mei 26, 1995, lakini kutokana na mvutano, umemeulianza kuzalishwa Januari 2002 na mkataba huo ni moja ya mikatabaambayo Kamati Teule ilipendekeza serikali iipitie upya.


Akijibu swali juu ya namna atakavyoshirikiana na Rostam wakiwa wanaCCM katika uchaguzi hata baada ya kuchafuana, alisema yeye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu sawa na Rostam.


“Muulizeni mwenyewe kwa nini anatuma vijana wake kuchafua wenzake analifikiriaje hilo!”


Aliviasa vyombo vya habari kutumia fursa walizonazo kuokoa taaluma hiyo ambayokwa mujibu wake, inaelekea pabaya, akitolea mfano alivyotumiwa kwenyebarua pepe, habari ya kummaliza, hali iliyomfanya atambue kuwa taalumahiyo imeingiliwa.


Alisema suala hilo lote ni jambo dogo, lakini limekuzwa kutokana namaslahi ya watu ambayo yangepaswa kujadiliwa bungeni.


“Tumelikuzakupita kiasi, issue (masuala) za Bunge zimalizikie bungeni na sikwenye magazeti yetu … ya bungeni yaishie bungeni.”


Kwa upande wake,Rostam alisema kwanza yeye si gazeti wala mwandishi wa habari na walahaelewi chochote ila kama Mwakyembe amekiri kumiliki kampuni ni kwelimgongano wa maslahi kwa vyovyote vile utakuwapo.


“Sitaki kuzungumza zaidi ila nasema mimi si mwandishi na kama Dk.Mwakyembe ameandikwa kwenye gazeti, basi ajibu hoja asianze kutafutawatu au kuwaandama,” alisema Rostam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad