HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 4, 2008

Mazishi Ya Aliyekuwa Rais Wa Zambia Dr.Levy Mwanawasa Yafanyika Jana Jijini Lusaka

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa pole Rais wa kwanza wa Zambia Dr.Keneth Kaunda wakati wa mazishi ya Rais wa Zambia Marehemu Dr. Levy Mwanawasa,yaliyofanyika jijini Lusaka Zambia jana.Rais Kikwete amerejea jijini Dar es Salaam jana jioni
Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitoa heshima katika kaburi la Rais wa Zambia Marehemu Levy Mwanawasa mara baada ya kuweka shada la maua katika kaburi hilo eneo la Embassy Park jijini LusakaRais wa Kwanza wa Zambia Dr. Kenneth Kaunda na Rais Mstaafu wa Tanzania Mh.Benjamin Mkapa wakifatilia Mazishi ya Rais wa Zambia Dr.Levy Mwanawasa.
Mjane wa aliyekuwa Rais wa Zambia,Mama Maureen Mwanawasa akiwaongoza wanae kwenda kuweka shada la maua katika kaburi la baba yao Marehemu Dr.Levy Patrick Mwanawasa aliyezikwa jana jijini Lusaka Zambia.
Askari wa jeshi la Zambia wakiwa wamebeba jeneza la Rais Wa Zambia Dr.Levy Mwanawasa tayari kwa mazishi yaliyofanyika katika viwanja vya Embassy Park, jijini Lusaka, Zambia jana.
Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na Mkewe Mama Anna Mkapa wakienda kuweka shada la maua katika kaburi la marehemu Dr.Levy Mwanawasa. picha zote ni kwa mujibu wa mdau Freddy Maro wa Ikulu



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad