Kiongozi wa Simba,Hassan Dalali(shoto) naye akipokea alichokabidhiwa mwenzake wa Yanga hapo juu.
Viongozi wa TBL,Yanga na Simba wakitia saini makubaliano ya udhamini huo
.Udhamini wa shilingi bilioni tatu kwa miaka mitatu
.Udhamini watoa motisha kushinda ligi kuu
.TBL yaendeleza azma yake ya kusaidia mpira wa miguu
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro Premium Lager inayo furaha kuwa mfadhili mkuu wa timu mbili kubwa kuliko zote ambazo pia ni injini za mpira katika historia ya Tanzania.
Ufadhili huu haulengi tu katika kuikuza bia ya Kilimanjaro Premium Lager lakini pia katika kuzisaidia timu hizi mbili kuendeleza mpira nchini Tanzania hasa ikizingatiwa kihistoria mchango wa timu hizi mbili katika michezo na maendeleo ya Tanzania kama taifa.
Ufadhili huu wa miaka mitatu una thamani ya Shilingi bilioni moja (1) kwa mwaka, ambayo jumla yake kwa miaka mitatu ni Shilingi bilioni tatu (3). Kila mwaka kiasi cha Shilingi milioni 654 kitaelekezwa kwa timu na zinazobakia kutumika kwenye shughuli za uendeshaji na uendelezaji wa ufadhili huu. Msaada huu pia unamaanisha kuwa iwapo mojawapo ya timu hizi itashinda Ligi Kuu ya Vodacom, itazawadiwa Shilingi milioni ishirini na tano (25); wakati nyingine itachukua kiasi cha Shilingi milioni kumi na tano (15) iwapo itakuwa mshindi wa pili. Timu hizi pia zitapatiwa Shilingi milioni ishirini na tano (25) kwa ajili ya usajili na Shilingi milioni kumi (10) kwa ajili ya kukarabati ofisi.
Akizungumzia uamuzi huu wa kihistoria, Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Bw. David Minja alisema, “TBL imechukua uamuzi huu wa kukumbukwa kama ishara ya kusimika azma yake ya kuhakikisha maendeleo ya michezo yanapewa kipaumbele cha hali ya juu. Simba na Yanga zinawakilisha uhai wa michezo nchini na tuliona sawa kabisa kuhusika moja kwa moja na nia ya kuziendeleza timu hizi.”
Minja aliongeza pia kuwa ufadhili wa timu hizi mbili utakuwa hasa ni kupata uzoefu wa kuwa sehemu ya mioyo ya watu wa jinsia zote mbili nchini Tanzania wanaoupenda mchezo wa soka, timu hizi mbili na taifa kwa ujumla.
Ufadhili huu pia unalenga katika kuzijenga na kuziendeleza timu hizi kwa kufanya yafuatayo:Kuzipatia msaada wa gharama za uendeshaji kwa mwaka mzima .Mishahara ya wachezaji pamoja na baadhi ya waongozaji wa timu Kuzipatia timu vifaa vya mazoezi pamoja na jeziKuzipatia timu mabasi Kuzitangaza timu hizi kupitia njia mbalimbali za mawasiliano.
Akielezea ufadhili huu mkubwa wa aina yake, Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager Bw. Oscar Shelukindo alisema, “Tunajivunia sana kutangaza ufadhili huu wa kihistoria na wa aina yake. Sisi, Kampuni ya Bia Tanzania, tunathamini michezo na yote ambayo michezo inawakilisha. Simba na Yanga zina mashabiki wengi mno nchi nzima na Kilimanjaro Premium Lager inajivunia kuwa sehemu yao.”
Simba na Yanga, timu kubwa na zinazojulikana kuliko timu yoyote nchini zimekuwa na historia ya upinzani na hivyo kujijengea himaya kubwa ya mashabiki ndani na nje ya nchi. Ushabiki huu umezifanya timu hizi kuwa kivutio cha wachezaji wanaochipukia wenye nia ya kufanikiwa kimpira. Wachezaji wengi wa Kitanzania wanaocheza mpira wa kulipwa nchi za nje wamewahi katika kipindi kimoja au kingine kuchezea moja ya klabu hizi.
Kwa upande wake, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Leodgar Tenga alisema, “Kwa mara nyingine tena TBL imedhihirisha imani iliyopo miongoni mwetu kuwa Simba na Yanga zinawakilisha sifa ya utaifa wetu. Kwa kuwafadhili mafahali hawa wawili Kilimanjaro Premium Lager siyo tu kwamba imewapa nafasi kubwa kuliko zote kujiendeleza bali pia imeinua roho ya kila mpenzi wa kweli wa mpira wa miguu.”
Kwa kuzifadhili timu hizi mbili, TBL inaendeleza azma yake ya kuuendeleza mpira wa miguu nchini kwa kumwaga kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya maendeleo ya mchezo huu. Mapema mwaka huu Safari Lager ilitoa Shilingi milioni mia sita (600) kwa ajili ya Taifa Cup, wakati Castle Lager hivi karibuni ilidhamini Kombe la Kagame kwa kiasi cha Shilingi milioni mia moja (100). Ufadhili huu kwa Simba na Yanga utazisaidia zaidi timu hizi kufanya vizuri kutokana na kuwa na vifaa bora, kuongezewa uwezo wa kujiamini pamoja na mazingira mazuri zaidi ya kimchezo. Ufadhili huu umekuja wakati muafaka ambapo wachezaji wa timu zote mbili sasa wanaweza kuonekana kimpira barani Afrika.
Kilimanjaro Premium Lager imeamua kwa moyo wote kuzifadhili timu hizi na kuhakikisha kuwa siyo tu zinakua, bali taifa zima pia linakua kimpira.
Kwa maelezo zaidi:
Oscar Shelukindo,
Kilimanjaro Brand Manager,
+255 767 266833,
Maneno Mbegu,
Corporate Communications Manager,
+255767266806,
Mabhe Matinyi, Silver Bullet,
Media Relations,
+255 712 785695,
No comments:
Post a Comment