
mbunifu wa mitindo anayekuja juu kwa kasi sana ally rhemtullah (pichani akiwa kabebwa na mamodo) mwezi ujao anatarajiwa kuweka rekodi katika historia ya wabunifu wa mitindo bongo,baada ya kualikwa kushiriki kwenye maonesho ya kimataifa ya LONDON FASHION WEEK.
akiwa ni mbunifu wa kwanza kualikwa kwenye maonesho hayo, ally anasema hata yeye ameshangaa kupata mualiko huo kwani ni ngumu kupata.
amesema hata wabunifu wa sauzi huwachukua miaka takribani 10 kupata mwaliko kama huo, lakini yeye amefanikiwa kupata nafasi hiyo japo ana miaka miwili tu kwenye gemu.
Hilo litakuwa bao la kisigino ambalo ally atakuwa amewapiga wabunifu wote wa bongo na ist afrika mashariki na globu hii inampa hongera inamtakia mafanikio zaidi...
bofya hapa pate mwandani wa ally rhemtullah
No comments:
Post a Comment