Nina furaha na fahari kuwafahamisha maendeleo ya mchakato wa kuundwa na hatimaye kusajili rasmi tawi la BongoReds a.k.a Bwawa la Maini ambapo wapenzi wote wa klabu ya Liverpool FC popote walipo wanakaribishwa kujiunga.
Hadi sasa wadau takriban 100 wamejitokeza kujiunga na tawi hili la Liverpool hapa bongo, na wengine ni kutoka mikoani na hata nje ya nchi. Kwa niaba ya kamati ya muda inayosimamia usajili huu natoa shukrani kwa wale wote waliotuma majina na maelezo yao kwa azma hiyo.
Hivi sasa kamati inajiandaa kutuma huko Anfield orodha ya majina hayo ambayo yatakuwa ya wanzilishi na kisha baada ya kusajiliwa zoezi la kusajili wapenzi wengine wa Liverpool litaendelea. Mwisho wa kupokea majina ya awali itakuwa ni siku ya Ijumaa saa sita kamili za mchana kwa saa za bongo.
Hii haimaanishi kwamba wataochelewa kutuma majina na maelezo yao watakuwa wamekosa nafasi. Hayo majina ya awali ni kutimiza sharti la kuwa na majina ya wanachama waanzilishi ili kuweza kupata usajili rasmi. Baada ya hapo zoezi litaendelea ili kupata wanachama wengi zaidi.
Wanakamati ya muda wamejitolea kugharamia zoezi zima la usajili ili kuharakisha mchakato huu. maelekezo ya kujiandikisha na hatimaye kupata kadi ya uanachama yatatolewa mara baada ya kupata usajili kamili toka huko Anfield.
Anuani yetu pepe ni bwawalamaini@gmail.com

Hivyo stay tuned....
YOU WILL NEVER WALK ALONE
PS: sio vibaya tukiwachunglia Liverpool wenzetu wa Dubai wanavyoendeleza libeneke kama hili tunalotaka kuanzisha kwa kubofya hapa

No comments:
Post a Comment