HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 20, 2026

TAEC YAJIIMARISHA MAANDALIZI YA TANZANIA KUTUMIA NYUKLIA KUZALISHA UMEME

 


Na Mwandishi Wetu
TUME ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) imesema Tanzania imeendelea kujiandaa kwa matumizi ya teknolojia ya nyuklia katika uzalishaji wa nishati ya umeme, ikiwa ni sehemu ya mikakati ya Serikali ya kuimarisha upatikanaji wa nishati nchini.

Akizungumza wakati wa warsha ya wataalamu kutoka TAEC, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Wizara ya Nishati iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Teknolojia na Huduma za Kiufundi wa TAEC, Dkt. Remigius Kawala, amesema maandalizi mbalimbali yamefanyika kuwezesha utekelezaji wa mpango huo.

Amesema hatua zilizofikiwa ni pamoja na kufanya tathmini za kiusalama pamoja na kujifunza uzoefu kutoka nchi zinazotumia teknolojia ya nyuklia kuzalisha umeme, ili Tanzania iweze kuzingatia viwango na taratibu zinazohitajika kabla na wakati wa matumizi ya teknolojia hiyo.

Dkt. Kawala amesema Serikali tayari imeweka mikakati ya kuelekea matumizi ya nishati ya nyuklia, huku TAEC ikiwa na jukumu la kuhakikisha mikakati hiyo inatekelezwa kwa kuzingatia usalama na utaalamu unaohitajika.

Amesisitiza kuwa ushirikiano wa wataalamu na taasisi mbalimbali zinazohusika na sekta ya nishati ni muhimu katika kuhakikisha Tanzania inakuwa tayari kutumia teknolojia ya nyuklia kwa usalama na ufanisi katika uzalishaji wa umeme.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad