HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, November 28, 2026

STAMICO YATOA MAFUNZO YA KUTUMIA NISHATI YA RAFIKI BRIQUETTES KWA WANA CHIGONGWE

 


*Dkt Mwasse awaasa washiriki wote kuwa mabalozi wa Rafiki Briquettes.

Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Madini la Taifa ( STAMICO) katika muendelezo wa kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya Rafiki Briquettes, imefanya mafunzo kwa wananchi wa Kata ya Msembeta, Chigongwe kwa kuwaonesha inavyozalishwa, Inavyowekwa kwenye vifungashio, Inavyowashwa na namna sahihi ya kuitunza na kuihifadhi.

Mafunzo hayo yamefanyika leo tarehe 28 Novemba 2026 katika Kiwanda cha Rafiki Briquettes kilichopo Chigongwe, Dodoma na kufunguliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt Venance Mwasse ambaye aliambatana na Menejimenti nzima, na watumishi kutoka ofisi za STAMICO makao makuu Dodoma na wale wa Dar es salaam

Akiongea kwa niaba ya wananchi wa Chigongwe, Diwani wa Kata hiyo Mhe William Nadoo ameishukuru STAMICO kwa kuchagua kuweka Kiwanda cha Nishati ya Rafiki Beiquettes katika Kata yao akiamini watu wa Chigongwe na maeneo ya karibu watapata kipaumbele katika fursa zote zinazohusu Kiwanda hicho.

Ameongeza yeye kama Diwani atahamasisha watu wa eneo hilo la Chigongwe watumie Nishati hii na amemuomba Mkurugenzi Mtendaji awapatie fursa vijana wa Chigongwe wawe mawakala wadogo watakaosambaza katika vituo mbalmbali ndani ya Kata ya Chigongwe.

Akiongea baada ya mafunzo hayo, Dkt Mwasse amemuahidi Mhe Diwani kutoa TOYO moja itakayosaidia kusambaza katika maeneo yote ya Chigongwe na amemuelekeza Meneja wa Masoko na Mahusiano kuhakikisha masuala yote ya vijana wa Chigongwe ambao Mhe Diwani atawatafuta pamoja na TOYO ya kuwasaidia kusambaza Nishati hiyo yakamilishwe mara moja.

Dkt Mwase amemuelezea Mhe Diwani kwamba tayari wataalamu wake wameshapokea ramani na gharama ya Darasa ambalo STAMICO imeahidi kujenga na atahakikisha darasa hilo linakamilika kwa haraka.

Dkt Mwase amemaliza kwa kuwaomba viongozi wa Kata ya Chigongwe, Menejimenti na wote waliohudhuria kuwa mabalozi wa Nishati hii ya Rafiki Briquettes kwasababu kwanza inatumia malighafi zote za hapa Tanzania, pili inalinda mazingira na afya za watu.


STAMICO, inaendelea kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi kuendelea kuunga juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita ya kuhakikisha matumizi ya Nishati Safi yanaongezeka ili ikifika mwaka 2034 yawe yamefikia asilimia 80.a Uhamasishaji wa matumizi ya Rafiki Briquettes kwenye jamii jirani na Viwanda

✅Dkt Mwasse awaasa washiriki wote kuwa mabalozi wa Rafiki Briquettes.

✅Awaahidi wana Chigongwe kupewa kipaumbele katika mradi huu wa Rafiki Briquettes

✅Atoa TOYO moja kusambaza Rafiki Briquettes katika maeneo yote ya Chigongwe.

Shirika la Madini la Taifa ( STAMICO) katika muendelezo wa kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya Rafiki Briquettes, imefanya mafunzo kwa wananchi wa Kata ya Msembeta, Chigongwe kwa kuwaonesha inavyozalishwa, Inavyowekwa kwenye vifungashio, Inavyowashwa na namna sahihi ya kuitunza na kuihifadhi.

Mafunzo hayo yamefanyika leo tarehe 28 Novemba 2026 katika Kiwanda cha Rafiki Briquettes kilichopo Chigongwe, Dodoma na kufunguliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt Venance Mwasse ambaye aliambatana na Menejimenti nzima, na watumishi kutoka ofisi za STAMICO makao makuu Dodoma na wale wa Dar es salaam

Akiongea kwa niaba ya wananchi wa Chigongwe, Diwani wa Kata hiyo Mhe William Nadoo ameishukuru STAMICO kwa kuchagua kuweka Kiwanda cha Nishati ya Rafiki Beiquettes katika Kata yao akiamini watu wa Chigongwe na maeneo ya karibu watapata kipaumbele katika fursa zote zinazohusu Kiwanda hicho.

Ameongeza yeye kama Diwani atahamasisha watu wa eneo hilo la Chigongwe watumie Nishati hii na amemuomba Mkurugenzi Mtendaji awapatie fursa vijana wa Chigongwe wawe mawakala wadogo watakaosambaza katika vituo mbalmbali ndani ya Kata ya Chigongwe.

Akiongea baada ya mafunzo hayo, Dkt Mwasse amemuahidi Mhe Diwani kutoa TOYO moja itakayosaidia kusambaza katika maeneo yote ya Chigongwe na amemuelekeza Meneja wa Masoko na Mahusiano kuhakikisha masuala yote ya vijana wa Chigongwe ambao Mhe Diwani atawatafuta pamoja na TOYO ya kuwasaidia kusambaza Nishati hiyo yakamilishwe mara moja.

Dkt Mwase amemuelezea Mhe Diwani kwamba tayari wataalamu wake wameshapokea ramani na gharama ya Darasa ambalo STAMICO imeahidi kujenga na atahakikisha darasa hilo linakamilika kwa haraka.

Dkt Mwase amemaliza kwa kuwaomba viongozi wa Kata ya Chigongwe, Menejimenti na wote waliohudhuria kuwa mabalozi wa Nishati hii ya Rafiki Briquettes kwasababu kwanza inatumia malighafi zote za hapa Tanzania, pili inalinda mazingira na afya za watu.

STAMICO, inaendelea kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi kuendelea kuunga juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita ya kuhakikisha matumizi ya Nishati Safi yanaongezeka ili ikifika mwaka 2034 yawe yamefikia asilimia 80.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad