HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 27, 2026

NIC INSURANCE YAIBUKA KIDEDEA TUZO ZA NBAA 2026

 


Na Mwandishi Wetu
NIC Insurance imeibuka mshindi wa Kwanza katika tuzo za uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za hesabu kwa kuzingatia Viwango vya Kimataifa vya Uhasibu kwa mwaka 2026, katika kipengele cha Kampuni zinazotoa Huduma za Bima nchini zilizoandaliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).

Akizungumza baada kupokea tuzo hiyo, Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano Karimu Meshack katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya APC, Bunju, jijini Dar es Salaam, amesema ushindi huo si jambo rahisi kutokana na uwepo wa kampuni nyingi za Bima zinazoshindana, lakini NIC Insurance imeendelea kudumisha ubora katika uandaaji na uwasilishaji wa taarifa zake za kifedha.

Amesema mafanikio hayo yanaonesha dhamira ya shirika hilo katika kutekeleza majukumu yake kwa weledi na uwazi, hatua inayochangia kujenga imani wateja wanaopata huduma za bima.

Ameeleza kuwa NIC Insurance imeendelea kufanya vizuri katika tuzo za NBAA kwa miaka mbalimbali katika kipengele cha Kampuni za Bima, jambo linaloonesha uimara wa mifumo yake ya usimamizi wa fedha na uwajibikaji.

Aidha, amesema tuzo hiyo ni kielelezo cha namna shirika hilo linavyotumia rasilimali lilizopewa na kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia misingi ya uwajibikaji, weledi na viwango vinavyokubalika kimataifa.

Ameongeza kuwa maendeleo endelevu katika sekta ya Bima nchini inahitaji kuwa na mifumo imara ya usimamizi wa fedha na kuzingatia misingi bora ya uhasibu ili kuimarisha uwazi na uwajibikaji.

Amesema uzingatiaji wa viwango vya kimataifa vya uhasibu ni muhimu kwa kuwa unaziwezesha taasisi kujenga uaminifu kwa wadau wa ndani na nje ya nchi, pamoja na kuimarisha ushirikiano na taasisi za kimataifa.

Ameongeza kuwa maendeleo endelevu katika sekta ya Biama inahitaji kuwa na mifumo imara ya usimamizi wa fedha na kuzingatia misingi bora ya uhasibu ili kuimarisha uwazi na uwajibikaji.

Amesema uzingatiaji wa viwango vya kimataifa vya uhasibu ni muhimu kwa kuwa unaziwezesha taasisi kujenga uaminifu kwa wadau wa ndani na nje ya nchi, pamoja na kuimarisha ushirikiano na taasisi za kimataifa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad