HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 27, 2026

MWENDA: KODI ZA WATANZANIA ZIKO SALAMA, ZINATUMIKA KWA MASLAHI YA UMMA

 



Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuph Juma Mwenda, amesema kodi zinazokusanywa na mamlaka hiyo ziko salama na zinatumika kwa maslahi mapana ya Watanzania, akisisitiza kuwa mafanikio hayo yanatokana na weledi, uadilifu na uzalendo wa watumishi wake.

Mwenda amesema hayo Novemba 26, 2026, katika Viwanja vya APC, Bunju, Dar es Salaam, baada ya kupokea tuzo ya mshindi wa jumla katika Tuzo za Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).

Amesema tuzo hiyo ni uthibitisho wa ubora wa watumishi wa TRA pamoja na usimamizi mzuri wa hesabu za taasisi hiyo, zinazojumuisha pia mapato yanayotokana na kodi za wananchi.

“Kwa sababu mahesabu yetu yamekuwa presented vizuri, na mahesabu tunayopresent ni pamoja na kodi za wananchi, maana yake kodi za Watanzania ziko salama na zinatumika kwa maslahi mapana ya wananchi wote,” amesema.

Amewapongeza walipa kodi na watumishi wa TRA kwa mchango wao katika mafanikio hayo, huku akiwataka Watanzania kuendelea kuwa na imani na taasisi hiyo.

Amesema TRA itaendelea kuboresha huduma kwa walipa kodi, kuwezesha biashara zao na kuhakikisha kodi zinazokusanywa zinawasilishwa Hazina kwa ajili ya kugharamia shughuli za umma na maendeleo ya wananchi.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad