Katika ziara hiyo, Mhe. Mchengerwa amepongeza uongozi wa hospitali hiyo kwa usimamizi mzuri wa hospitali na kwa ubora mkubwa wa huduma za kibingwa na kibobezi zinazotolewa kwa wananchi na kubainisha kuwa Muhimbili-Mloganzila imekuwa nguzo muhimu na ya kimkakati katika sekta ya matibabu nchini.
Pamoja na kutoa pongezi hizo, Waziri Mchengerwa ametumia fursa hiyo ya kipekee kuzungumza na wananchi waliofika kupata huduma.
Mhe. Mchengerwa amesisitiza kuwa lengo kuu la ziara hiyo ni kujadili kwa pamoja namna ya kuimarisha mifumo ya utendaji kazi na kujenga misingi thabiti ya uwajibikaji wa pamoja na kuongeza kuwa ni lazima kila mtumishi ahakikishe wagonjwa wanapata huduma bora, zenye hadhi na heshima bila kukumbana na vikwazo vyovyote visivyo vya lazima.
"Mifumo yetu ya utendaji kazi lazima iimarishwe ili kujenga misingi thabiti ya uwajibikaji. Tunataka wananchi wapate huduma bora na za heshima bila vikwazo," amesema Waziri Mchengerwa
Hatua hii ya Waziri inakuja wakati Wizara ya Afya ikiwa imedhamiria katika kutekeleza mikakati endelevu inayolenga kuhakikisha Taasisi zote za Afya za Umma nchini zinajenga imani kubwa kwa wananchi kupitia utoaji wa huduma zenye kiwango na hadhi ya kitaifa na kimataifa.

.jpeg)
No comments:
Post a Comment