HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, November 14, 2026

MARANJE KUWA KITOVU CHA UCHAKATAJI WA KOROSHO TANZANIA

 







MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Deogratius John Ndejembi ameweka rasmi jiwe la msingi la ujenzi wa Mradi wa Kongani la Viwanda tarehe 13 Novemba 2026, katika Kijiji cha Maranje, Halmashauri ya Nanyamba mkoani Mtwara.

Hafla hiyo imefanyika katika eneo la mradi unaosimamiwa na Wizara ya Kilimo kupitia Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya Makamu wa Rais mkoani Mtwara na kukagua na kuhamasisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo yenye manufaa kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Katika tukio hilo, Mhe. Ndejembi ameambatana na Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo (Mb), pamoja na Viongozi wengine wa Serikali.

Mradi huo wa kimkakati wa Kongani la Viwanda Maranje unalenga kujenga miundombinu ya kisasa ya viwanda vya kubangua na kuongeza thamani ya zao la Korosho hapa nchini. Mradi huo unatarajiwa kuchochea ukuaji wa uchumi wa mkoa wa Mtwara, kuongeza kipato cha wakulima na kuzalisha maelfu ya ajira kwa vijana na wananchi wa Nanyamba na maeneo ya jirani.

Kupitia uzinduzi huo, Makamu wa Rais ameelekeza bomba la gesi kufikishwa katika Kongani hiyo, na pia kuagiza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuweka miundombinu mahsusi ya umeme ili kuhakikisha upatikanaji wa Nishati ya uhakika kwa shughuli za viwanda.

Aidha, Makamu wa Rais amekabidhi mashine 100 za kısasa zinazotumia umeme kwa ajili ya kuwawezesha wabanguaji wadogo kuongeza ufanisi wa uzalishaji. Kila mashine ina uwezo wa kubangua kilo 700 za Korosho kwa siku, hivyo mashine zote 100 zilizokabidhiwa na Makamu wa Rais zina uwezo wa kubangua kilo 70,000 kwa siku. Hatua hiyo inatarajiwa kufungua zaidi ya ajira zaidi 4000 kwa wakazi wa Mtwara, hususan vijana.

Uzinduzi wa Mradi wa Kongani la Viwanda Maranje unaashiria hatua muhimu katika juhudi za Serikali za kuongeza thamani ya mazao ya kimkakati, kuimarisha uchumi wa viwanda na kuinua ustawi wa wakulima wa Korosho nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad