Brenda Callixte Kanamugile kutoka Mkoa wa Morogoro, ameibuka mshindi wa shindano la Miss Tanzania Eastern Zone 2026 na kujinyakulia zawadi ya gari aina ya Mazda Verisa.
Brenda amewashinda washiriki wengine 13 kutoka mikoa minne inayounda Kanda ya Mashariki ambayo ni Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara katika fainali zilizofanyika Novemba 6, 2026, Kisemvule, Wilaya ya Mkuranga, Mkoa wa Pwani.
Baada ya kukamilika kwa mashindano ya ngazi ya kanda, Brenda anaingia kambini kuungana na washindi kutoka kanda nyingine zinazounda Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya kumpata Miss Tanzania 2026


No comments:
Post a Comment