DAR ES SALAAM, 25 Novemba 2026.
KATIKA kipindi hiki cha likizo ambapo familia zinapata muda zaidi wa kuwa pamoja, Airtel Tanzania kwa kushirikiana na Huawei inasogeza huduma ya intaneti ya kasi ya Airtel Fiber karibu na kaya katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam na Arusha.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Airtel Fiber katika eneo la Makumbusho, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Charles Kamoto, akiwa pamoja na Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Saad Mtambule, alisema kuwa wateja na wananchi watapata fursa ya kufahamu zaidi huduma hiyo, kujionea uwezo wake, na kuelewa jinsi intaneti ya uhakika inavyoweza kukidhi mahitaji ya kidijitali ya familia za kisasa.
Airtel, ambayo ni kinara wa huduma za intaneti ya nyumbani nchini Tanzania, inaendelea kupanua wigo wa mtandao wake wa fiber (Fibre-to-the-Home - FTTX) ili kusogeza huduma ya intaneti ya kasi karibu na makazi, ofisi, na maeneo ya biashara. Kwa sasa, huduma ya Airtel FTTX inapatikana katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam, yakiwemo Mikocheni, Goba Matosa, Mbezi Beach, Kinyerezi, Makumbusho, pamoja na maeneo ya Kigamboni, Nunge, OctoPrime, na KKKT Vijibweni, na Moshono jijini Arusha.
Hatua muhimu katika upanuzi huu ni kuzinduliwa rasmi kwa mtandao wa Airtel FTTX katika eneo la Makumbusho, ambako miundombinu hiyo ina uwezo wa kufikia majengo 2,500 (Home Passes), na hivyo kutoa fursa kwa hadi kaya, ofisi, na biashara 2,500 kuunganishwa na huduma ya intaneti ya kasi ya Airtel Fiber
Katika kipindi cha likizo, matumizi ya intaneti majumbani huongezeka kutokana na watoto kuwa nyumbani na familia kutumia muda mwingi pamoja, hali inayofanya intaneti ya uhakika kuwa muhimu kwa burudani, mawasiliano, elimu, na kazi. Ili kukidhi mahitaji hayo, Airtel Fiber inatoa vifurushi visivyo na kikomo (Unlimited) vyenye kasi ya hadi Mbps 100 na Mbps 200 (kuanzia TSh 70,000 na TSh 100,000, vinavyowezesha familia kutazama video mtandaoni, kucheza michezo ya kidijitali, kujifunza, na kufanya kazi wakiwa nyumbani kwa ufanisi bila changamoto za video kukwama au mawasiliano kukatika.
Akizungumzia hatua hiyo, Charles Kamoto, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, alisema kampuni inaendelea kuwekeza katika teknolojia ya kisasa ili kusogeza intaneti ya uhakika karibu na wananchi na kuwawezesha kunufaika na mabadiliko ya kidijitali.
“Tanzania inapitia mabadiliko makubwa ya kidijitali, na kiini cha mabadiliko hayo ni upatikanaji wa intaneti ya uhakika. Kupitia Airtel Fiber, tunasogeza teknolojia ya kisasa karibu na wakazi wa Makumbusho, kwa kasi ya Mbps 100 na Mbps 200 kulingana na mahitaji ya mteja. Tunataka familia na biashara zinufaike na mawasiliano ya kasi yanayorahisisha maisha, kazi na shughuli zao za kila siku,” alisema Kamoto.
Ili kufanya huduma hiyo ipatikane kwa urahisi zaidi, Airtel inatoa ofa ya Double Benefit Impact with Airtel Fiber, inayowawezesha wateja wapya kupata ofa ya mwezi mmoja wa intaneti bila malipo wanapojisajili kwa mara ya kwanza na kuchagua kifurushi chenye thamani ya kati ya Shilingi 70,000 na Shilingi 100,000. Ofa hii inawapa wateja nafasi ya kufurahia intaneti ya kasi ya nyumbani huku wakipata thamani zaidi ya huduma wanayolipia.
Ofa hiyo inakuja wakati muafaka kwa familia zinazotaka kufurahia burudani pamoja, kuwawezesha watoto kutumia rasilimali za kujifunzia mtandaoni, kuwasiliana na ndugu na marafiki, pamoja na kuendelea na shughuli za kazi na biashara wakiwa nyumbani katika kipindi hiki cha likizo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Saad Mtambule, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na Mgeni Rasmi, aliipongeza Airtel Tanzania na Huawei kwa kusogeza huduma ya intaneti ya kasi karibu na wananchi, akieleza kuwa mawasiliano ya uhakika yana mchango muhimu katika maendeleo ya jamii na uchumi.
“Intaneti ya kasi na ya uhakika ni muhimu kwa maendeleo ya jamii na uchumi. Kupitia Airtel Fiber, wafanyabiashara wa Makumbusho watapata fursa ya kutangaza bidhaa zao mtandaoni, kuwafikia wateja wengi zaidi na kuendesha biashara zao kwa ufanisi. Ninawahimiza wananchi kutumia huduma hii na kunufaika na fursa za uchumi wa kidijitali,” alisema Mhe. Mtambule.
Kupitia ushirikiano wake na Huawei, Airtel inaendelea kuimarisha huduma zake za intaneti ya nyumbani kwa kutumia teknolojia na miundombinu ya kisasa inayolenga kuwapatia wateja intaneti ya kasi na huduma bora zaidi.
Franklin Huang, Makamu wa Rais wa Huawei Tanzania, alisema ushirikiano huo unaonesha umuhimu wa kuunganisha utaalamu wa kiteknolojia na miundombinu ya mawasiliano ili kusogeza intaneti ya kasi karibu na kaya na biashara nyingi zaidi.
“Intaneti imekuwa muhimu katika kujifunza, kufanya kazi, kuwasiliana na kukuza biashara. Kupitia ushirikiano wetu na Airtel Tanzania, tunatoa teknolojia inayosaidia kupanua miundombinu ya nyuzi za mawasiliano na kusogeza intaneti ya kasi karibu na kaya na biashara nyingi zaidi. Tunajivunia kushirikiana na Airtel katika kujenga Tanzania iliyounganishwa zaidi,” alisema Bw. Huang.
Kadri Watanzania wanavyozidi kutumia teknolojia katika shughuli zao za kila siku, Airtel Tanzania inaendelea kujizatiti kupanua upatikanaji wa intaneti ya nyumbani na kuwawezesha wananchi kunufaika na fursa za elimu, biashara, mawasiliano na burudani zinazopatikana kupitia huduma za kidijitali.
Likizo hii, wasogeze familia na marafiki karibu zaidi kwa Airtel Fiber. Furahia kasi. Furahia mawasiliano. Furahia mengi zaidi na Airtel Fiber.




No comments:
Post a Comment