HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 14, 2026

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI IBADA YA KUMUOMBEA BABA WA TAIFA MWL. JULIUS KAMBARAGE NYERERE

  







Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, leo Oktoba 14, 2026, ameshiriki Ibada ya Misa Takatifu ya Kumbukizi ya Miaka 27 ya kifo cha Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Epifania, Jimbo Katoliki la Sumbawanga, mkoani Rukwa.

Ibada hiyo imeongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Sumbawanga, Mhashamu Damian Kyaruzi, na kuhudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba; Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere; Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Makongoro Nyerere, pamoja na viongozi mbalimbali, waumini na wananchi.

Ibada hiyo ni sehemu ya kumuenzi na kumkumbuka Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliyefariki dunia Oktoba 14, 1999.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi akisalimiana na Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere mara baada ya kushiriki Ibada ya Misa Takatifu ya Kumbukizi ya Miaka 27 ya kifo cha Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Epifania Jimbo Katoliki Sumbawanga, leo Oktoba 14 2026.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi akiwa Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba na Mkewe Mama Neema Nchemba, katika picha ya pamoja na Askofu Damian Kyaruzi, Mapadre pamoja na familia ya Baba wa Taifa Hayati. Mwl. Julius Kambarage Nyerere, mara baada ya kushiriki Ibada ya Misa Takatifu ya Kumbukizi ya Miaka 27 ya kifo cha Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Epifania Jimbo Katoliki Sumbawanga, leo Oktoba 14 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi akiwa katika picha ya pamoja na familia ya Baba wa Taifa Hayati. Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambao ni Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Makongoro Nyerere mara baada ya kushiriki Ibada ya Misa Takatifu ya Kumbukizi ya Miaka 27 ya kifo cha Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Epifania Jimbo Katoliki Sumbawanga, leo Oktoba 14 2026.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad