HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 7, 2026

MAANDALIZI YA KUKABILIANA NA MVUA ZA EL-NINO - TANROADS GEITA


Kaimu Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Geita, Mhandisi Hosea Machaka, amesema TANROADS inaendelea kuchukua hatua za maandalizi kukabiliana na mvua za El-Nino, ikiwemo kukagua barabara, madaraja na mitaro na kubaini maeneo hatarishi.

 

TANROADS Geita inasimamia jumla ya kilomita 1,019.13 za barabara, zikiwemo kilomita 708.08 za barabara za mkoa, 232.18 za barabara kuu na 78.87 za barabara za wilaya zilizokasimiwa, pamoja na madaraja 324.


Mhandisi Machaka amesema katika Barabara ya Katoro – Ushirombo, eneo la Daraja la Nyikonga, imefanyika kazi ya kufungua midomo ya daraja, kusafisha njia ya mto na kuelekeza mkondo wa maji (river training) ili kuboresha mtiririko. Katoro, mitaro imechimbwa kuelekeza maji maeneo salama, huku katika Barabara ya Mtakuja–Bukoli, eneo la Nyarugusu, kuta na mitaro vikifanyiwa kazi kuzuia maji kuvuka barabara.


Amesema pia katika Barabara ya Shinyanga – Kagera, eneo la Runzewe, uwezo wa daraja dogo umeongezwa ili kuboresha upitishaji wa maji. Geita Mjini, ujenzi wa mtaro mkubwa unaendelea kuanzia Stand Kuu kupitia Shelabela hadi Leni Hotel kwa ajili ya kuelekeza maji mtoni.

 

Aidha, TANROADS imepokea makalavati ya chuma aina ya Corrugated Metal Pipe (CMP) na ya plastiki aina ya PVC, huku mikataba ya matengenezo ikiwa imesainiwa na wakandarasi wakiwa katika maeneo ya kazi.


Wafanyakazi wamepewa mafunzo ya kukabiliana na dharura, na shughuli za ufuatiliaji na utatuzi wa changamoto zinafanyika kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

 

Kwa upande wake, Msimamizi wa Kitengo cha Mipango TANROADS Geita, Mhandisi Sabato Manyinyi, amesema ongezeko la shughuli za kilimo na makazi limeongeza mtiririko wa maji kuelekea barabarani, hali inayoweza kuathiri usafiri.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad