HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, August 1, 2026

WATUMISHI WA BUNGE WAIPONGEZA PSSSF KWA HUDUMA ZA KIDIJITALI

 

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji PSSSF, Bw. Hajji Moshi, akizungumza wakati wa semina maalum ya kutoa elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa Makatibu wa Kamati za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iliyofanyika mjini Morogoro tarehe 31 Julai, 2026.

Mmoja atoa ushuhuda wa ‘Tunalipa Jana’

Bunge: tunawashukuru PSSSF kwa elimu

Morogoro, Julai 31, 2026

Watumishi wa idara ya Kamati za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameridhishwa na huduma zinatolewa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa watumishi wa Umma (PSSSF) na wameshauri PSSSF izidishe ubunifu ili kurahisisha huduma kwa Wanachama wake.

Kauli hiyo imetolewa Julai 31, 2026 mjini Morogoro katika semina iliyoendeshwa na PSSSF maalum kwa Watumishi wa Bunge ambayo iliwashirikisha Makatibu wote wa kamati za Bunge. Semina ilikuwa ya kuwajengea uwelewa wa Kinga ya Jamii, hususani PSSSF.

“Hongereni sana matumizi ya mtandao hivi sasa mambo mmeyarahisisha sana, kwani kila kitu kinaanzwa na kumalizwa kwenye simu au kifaa kingine chochote cha kidijitali” alisema Bi. Angelina Sanga.

Mtumishi kutoka Ofisi ya Bunge, Bi. Angelina Sanga (kushoto), akiwa na Afisa Matekelezo kutoka PSSSF, Bi. Upendo Chilewa, wakati wa semina hiyo mjini Morogoro. Bi. Sanga alipokuwa akijisajili kaaika huduma ya mifumo ya kidijitali.

Aidha, wajumbe wa semina hiyo walishauri sera ya Kinga ya Jamii ipitiwe ili iweze kwenda na wakati.

Katika semina hiyo Mtumishi Mstaafu wa Bunge Bw. Gerald Magili alithibitisha kuwa PSSSF ‘inalipa jana’ kwa kusema, “Nilitoa taarifa ya kuomba kibali cha kustaafu kwa mwajiri miezi sita kabla ya kusataafu, tarehe yangu ya kustaafu ilikuwa ni Juni 25, 2026, siku hiyo hiyo nilipokea mafao yangu ya kustaafu, hakika PSSSF mpo vizuri”.


Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Kamati za Bunge, Bw. Michael Chikokoto, akizungumza wakati wa semina hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Bunge kwa ajili ya Makatibu wa Kamati za Bunge mjini Morogoro.

Akizungumza wakati wa kufunga semina hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa PSSSF, Bw. Hajji Moshi alishukuru ofisi ya Bunge kwa kutoa nafasi ya kufanyika semina hiyo na kusema kuwa Mfuko uko tayari wakati wowote kutoa elimu ya Kinga ya Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Bunge na Wanachama wengine

Mtumishi Mstaafu wa Bunge, Bw. Gerald Magili, akitoa ushuhuda wake wakati wa semina hiyo mjini Morogoro. Bw. Magili aliipongeza PSSSF kwa kulipa mafao yake kwa wakati

“Kwa niaba ya Menejimenti ya PSSSF, tunashukuru kupokea maoni kutoka kwenu, yote tumeyachukua na tutayafanyia kazi na yale ya Kisera tutayafikisha kwa Mamlaka husika, asanteni sana” alisema Bw. Hajji Moshi.

Kwa upande wake, Bw. Michael Chikokoto, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Kamatii za Bunge, alisema, “Tunawashukuru PSSSF kwa kuitikia wito wetu, naamini tumejifunza mengi na tatakuwa mabalozi wenu kwa watumishi wengine wa Bunge.


Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji PSSSF, Bw. Hajji Moshi (kushoto), akikabidhi zawadi kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Kamati za Bunge, Bw. Michael Chikokoto (kulia), mara baada ya kuhitimishwa kwa semina ya kutoa elimu ya Hifadhi ya Jamii iliyoandaliwa na Ofisi ya Bunge mjini Morogoro.

Makatibu wa Kamati za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia kwa umakini mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji PSSSF, Bw. Hajj Moshi (kulia), wakati wa semina ya kujenga uelewa wa Hifadhi ya Jamii iliyoandaliwa na Ofisi ya Bunge mjini Morogoro tarehe 31 Julai, 2026.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad