Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akikata utepe pamoja na Rais wa Jamhuri ya Angola Mheshimiwa João Manuel Gonçalves Lourenço kama ishara ya uzinduzi wa Hospitali Kuu ya Rufaa ya Rais Julius Nyerere (Hospital dos Queimados Presidente Julius Nyerere) iliyopo Kilamba, jijini Luanda, Angola, tarehe 01 Agosti, 2026. Kulia ni Mama Maria Nyerere, Mjane wa Baba wa Taifa akishuhudia tukio hilo. Hospitali hiyo imepewa jina la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kama heshima na ishara ya kutambua mchango wake katika harakati za ukombozi wa Bara la Afrika, hususan nchi za Kusini mwa Afrika, ikiwemo Angola.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Jamhuri ya Angola, Mheshimiwa João Manuel Gonçalves Lourenço, Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere pamoja na viongozi mbalimbali wakati wakifuatilia Makala Maalum ya Hospitali Kuu ya Rufaa ya Rais Julius Nyerere (Hospital dos Queimados Presidente Julius Nyerere) pamoja na Historia ya Baba wa Taifa kabla ya uzinduzi wa Hospitali hiyo iliyopo Kilamba, jijini Luanda, Angola, tarehe 01 Agosti, 2026.
Taswira ya Hospitali Kuu ya Rufaa ya Rais Julius Nyerere (Hospital dos Queimados Presidente Julius Nyerere) iliyopo Kilamba, jijini Luanda, nchini Angola.
Taswira ya Hospitali Kuu ya Rufaa ya Rais Julius Nyerere (Hospital dos Queimados Presidente Julius Nyerere) iliyopo Kilamba, jijini Luanda, nchini Angola.



.jpeg)


.jpeg)
No comments:
Post a Comment