Shirima alisema suluhisho za malipo ya mtandaoni za NMB pamoja na NMB SME World Business Credit Card zinalenga kurahisisha miamala ya ndani na nje ya nchi. Pia alisema NMB imeboresha huduma za Bank Guarantee, ambapo dhamana za zabuni zisizohitaji dhamana ya mali (Unsecured Bid Bonds) zinaweza kufikia hadi dola milioni 10 za Marekani bila kuweka dhamana ya mali.
Kwa upande wake Leah Mwakang’ata, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Biashara kwa Wateja Wadogo na wa Kati (SME) wa NMB, aliwahimiza wafanyabiashara kutenganisha fedha binafsi na fedha za biashara kupitia akaunti rasmi. Alisema hatua hiyo inawasaidia wafanyabiashara kufuatilia mapato na matumizi kwa usahihi, kujenga historia nzuri ya kifedha na kupata huduma za kifedha zinazokidhi mahitaji ya biashara zao.
Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Mwanza, Gabriel Mugini, alisema mazingira ya biashara mkoani humo yanaendelea kuvutia wawekezaji. Aliwataka wafanyabiashara kutumia fursa za kifedha na kiteknolojia zinazopatikana ili kupanua shughuli zao.



No comments:
Post a Comment