HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 3, 2026

NBAA YAENDELEA KUTOA ELIMU NANENANE


Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imeendelea kusogeza huduma zake karibu na wananchi kwa kushiriki Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo (Nanenane) 2026 yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. John Samuel Malecela, Nzuguni, jijini Dodoma.

Kupitia banda la NBAA, wananchi, wanafunzi, wahitimu na wadau mbalimbali wanapata fursa ya kujifunza kuhusu Taaluma ya Uhasibu, pamoja na kupata huduma mbalimbali za kitaaluma zinazotolewa na Bodi.

Huduma zinazotolewa katika banda hilo ni pamoja na usajili wa mitihani kuanzia ngazi ya chini "Accounting Technician" (ATEC) hadi ngazi ya Taaluma "Profesion" yaani CPA. Pia usajili wa uhamaji wa madaraja kwenda ACPA, ACPA-PP na FCPA au FCPA - PP pamoja na hayo wanatoa elimu juu ya usajili wa kampuni za Uhasibu na Ukaguzi, kozi za muda mfupi, pamoja na ushauri kuhusu fursa mbalimbali zinazotolewa na NBAA.

Aidha, wanafunzi wanaotamani kujiunga na Taaluma ya Uhasibu watapatiwa elimu kuhusu hatua za kuanza safari ya kuwa Wahasibu na Wakaguzi wa hesabu waliosajiliwa.

Ushiriki wa NBAA katika maonesho hayo ni sehemu ya jitihada za Bodi za kuendelea kuwafikia wananchi, kuongeza uelewa kuhusu huduma zake na kuhamasisha vijana wengi zaidi kujiunga na Taaluma ya Uhasibu ili kuchangia maendeleo ya uchumi wa nchi.

Maonesho ya Nanenane 2026 yanaendelea na kaulimbiu ni "Tambua Soko, Ongeza Tija, Kuendeleza Dira ya Taifa 2050." NBAA imewahimiza wananchi kutembelea banda lake lililondani ya Banda la Wizara ya Fedha ili kupata elimu, ushauri wa kitaaluma na huduma mbalimbali zinazotolewa na Bodi.
Watumishi wa NBAA wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Nanenane 2026 yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. John Samuel Malecela, Nzuguni, jijini Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa NBAA, Magreth Kageya akitoa elimu kwa mwananchi aliyetembelea Banda la Bodi hiyo katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Nanenane 2026.
Mfanyakazi wa NBAA Happiness Mwamwembe akitoa elimu kwa wananchi waliofika katika Banda la Bodi hiyo katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Nanenane 2026
Picha mbalimbali zikionyesha shughuli zinazoendelea katika banda la NBAA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad