HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 17, 2026

MUHAS Yaandaa Shule Ya Wahudumu Wa Huduma Za Dharura

 



Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv
CHUO Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kinaandaa mpango wa kuanzisha mafunzo ya wahudumu wa huduma za dharura watakaotoa huduma ya kwanza, ikiwemo usimamizi wa ajali, kuhakikisha njia ya hewa inabaki wazi na kumstabilisha mgonjwa kabla ya kufikishwa hospitalini.

Makamu Mkuu wa MUHAS, Prof. Apollinary Kamuhabwa, amesema hayo leo Agosti 18, 2026, Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kitengo maalumu cha matibabu ya meno kwa watoto wanaohitaji dawa za usingizi au ganzi, sambamba na kusainiwa kwa hati ya makubaliano (MoU) kati ya MUHAS, Chuo Kikuu cha Ankara na Shirika la Ushirikiano na Uratibu la Türkiye (TİKA).

Amesema mpango huo ni sehemu ya ushirikiano katika huduma za tiba za dharura, ambapo MUHAS imepokea gari la wagonjwa linalotumika kutoa huduma na kuwafundisha wanafunzi.

Amesema chuo hicho kinaandaa mpango wa kuanzisha mafunzo ya wahudumu wa huduma za dharura watakaotoa huduma ya kwanza, ikiwemo usimamizi wa ajali, kuhakikisha njia ya hewa inabaki wazi na kumstabilisha mgonjwa kabla ya kufikishwa hospitalini.

Alisema mpango huo ni muhimu zaidi wakati Tanzania, Kenya na Uganda zikijiandaa kwa pamoja kuandaa Fainali za AFCON 2027.

Mkurugenzi wa TİKA nchini Tanzania, Halim Ömer, amesema mpango wa kuanzisha shule ya wahudumu wa huduma za dharura utajengwa juu ya mafunzo ya kukabiliana na majanga na dharura yaliyotolewa mwaka 2024, ambapo zaidi ya madaktari 50 wa huduma za dharura walipatiwa mafunzo.

Amesema shule hiyo itasaidia kuandaa wataalamu wenye sifa na kuimarisha uwezo wa Tanzania wa kukabiliana na dharura kwa muda mrefu.

Ömer amesema TİKA imetekeleza zaidi ya miradi 350 ya ushirikiano nchini Tanzania katika sekta mbalimbali, ikiwemo elimu, kilimo, mifugo, afya, mafunzo ya ufundi, maji na usafi wa mazingira.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ankara, Prof. Dkt. Necdet Ünüvar, amesema ushirikiano katika tiba za dharura ni hatua muhimu katika kuimarisha uhusiano wa kitaaluma na kitaalamu kati ya taasisi hizo, huku akiahidi kupanua ushirikiano katika sayansi za afya.

Prof. Kamuhabwa amesema MoU iliyosainiwa haijaweka kiwango maalumu cha fedha, bali imeweka msingi wa taasisi hizo kuandaa na kutekeleza miradi ya pamoja na kutafuta fedha kutoka TİKA na washirika wengine wa maendeleo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad