HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 3, 2026

MHE. MARIAM ABDALLAH IBRAHIM AENDELEA NA ZIARA YA KUIMARISHA UHAI WA JUMUIYA MKOA WA MOROGORO

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Mhe. Mariam Abdallah Ibrahim, ameendelea na ziara yake katika Mkoa wa Morogoro, Wilaya ya Mvomero.


Akiwa Wilayani Mvomero, Mhe. Mariam amewashukuru wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na wananchi kwa kukiamini chama na kukipa ushindi mkubwa katika Uchaguzi Mkuu.

Katika ziara hiyo, amesisitiza umuhimu wa kuimarisha uhai wa jumuiya kwa kufanya vikao mbalimbali, kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika shughuli za chama, pamoja na kuwahimiza wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama.

Aidha, Mhe. Mariam amekagua vikundi vilivyopatiwa mikopo kupitia Halmashauri na kuangalia maendeleo ya miradi yao. Pia amekagua ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa UWT na kuchangia kiasi cha Shilingi Milioni Tano (5,000,000) kwa ajili ya kuunga mkono ujenzi huo.

“Tunaendelea kuimarisha jumuiya, kuwawezesha wanawake na kuhakikisha maendeleo yanafika kwa wananchi.”

Mhe. Mariam Abdallah Ibrahim
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT Taifa






 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad