HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 13, 2026

Mabadiliko Ya Sheria Za Kodi Yaleta Matumaini Kwa Wafanyabiashara Kagera

 


Na Mwandishi Wetu.
MAMLAKA ya Mapato Tanzania imeendelea kutoa mafunzo kuhusu mabadiliko ya sheria za kodi kwa mwaka wa fedha 2026/2027, yaliyoanza kutekelezwa Julai 1, 2026 yakilenga kuwawezesha mawakala, wadau wa forodha na watumishi wa mamlaka kuelewa misamaha na taratibu mpya za kodi pamoja na kupanua wigo wa biashara nchini.

Akifungua mafunzo hayo Mkoani Kagera Meneja wa TRA mkoani humo Joseph Mtalemwa amesema utekelezaji wa sheria hiyo unatarajiwa kukuza biashara hususani wawekezaji waliokuwa wakisubiri kupata misamaha ya kodi.

Amesema mafunzo hayo yatafanyika katika maeneo muhimu ya biashara na mipakani ikiwemo Mutukula, Rusumo, Kabanga na Bandari ya Bukoba.
Kwa upande wao, wawezeshaji wa mafunzo hayo Hassan Minga ambaye ni Afisa Mfawidhi wa Forodha Mkoa wa Dodoma na Allan Maduhu afisa Forodha mkuu wamesema baadhi ya mabadiliko hayo yanahusu misamaha kwenye vifaa vya kuchajia vyombo vya moto vinavyotumia nishati ya umeme ili kukuza matumizi ya nishati safi, pamoja na sekta ya uvuvi, ambapo kuna msamaha wa kodi kwenye nyuzi zinazotumika kuzalisha nyavu za kuvulia samaki.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo Marco Gabriel ambaye ni Mwenyeki wa Chama cha Mawakala wa Forodha mpakani Mutukula na Godwin Idan wamepongeza TRA mpango wake wa kutoa elimu ya mabadiliko ya sheria za kodi kwa wadau wote kwani inawasaidia wafanyabiashara kuelewa mabadiliko ya sheria na kutekeleza wajibu wao kwa usahihi, na kusaidia katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwa pamoja.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad