HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 11, 2026

KAMISHNA WA MAGEREZA AIPONGEZA NA KUISHUKURU STAMICO KWA USHIRIKIANO

 


Shirika la Madini la Taifa ( STAMICO) katika muendelezo  wa kuhakikisha linaendelea kuwa kinara  katika kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi Tanzania nzima, leo tarehe 11/8/2026  imeingia mkataba mnono  wa pande tatu kati ya  STAMICO, Chuo cha Mafunzo  na taasisi ya FDH  ya kuhakikisha magereza yote ya Zanzibar  yanaanza kutumia Nishati ya Rafiki  Briquettes.

Makubaliano hayo yamefanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar  na kushuhudiwa  na Kamishna  wa Magereza  Zanzibar Khamis Abdalah Khamis pamoja na  Mkurugenzi  Mtendaji  wa STAMICO  Dkt Venance  Mwasse na  Mkurugenzi  wa FDH  Bwn Michael Salali.

Akiongea katika hafla hiyo, Dkt Mwasse ameipongeza  taasisi ya FDH kwa kufanikisha kuingia makubaliano  haya ambayo yatawezesha Magereza  zote za Zanzibar  kupata Nishati hii ya Rafiki Briquettes  ambayo  inaenda kuleta afueni kwenye  gharama za Nishati kwa Magereza   lakini pia kuanza kutekeleza agenda ya Nishati Safi kwa taasisi zote zinazohudumia watu zaidi ya 100.

"Suala la Nishati Safi ni  Agenda ya Kitaifa na sisi STAMICO  tumeibeba kwa mikono miwili kuhakikisha tunatumia Nishati yetu ya Rafiki Briquettes  kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi" amesema Dkt Mwasse 

Dkt Mwasse  pia ameahidi kusaidia kuleta mafunzo na Kongamano  la  kuhamasisha  matumizi  ya Nishati Nzima kwa Watumishi wa Magereza na Wananchi wote wa Zanzibar.

Awali akiongea na kutoa salamu kutoka FDH, Bwn Salali ameahidi kuhakikisha  taasisi yake kwa kushirikiana  na STAMICO  itahakikisha Nishati hii inafika kwenye  Magereza  yote kwa wingi na inafika katika ubora unaostahili.

Naye, Kamishna Khamis ameishukuru na kuipongeza STAMICO  kwa kuhakikisha Nishati hii inafika  Zanzibar.

Ameomba pia STAMICO  iangalie kuwapa fursa hii  ya kusambaza  Nishati hii kwa wale  wafungwa ambao wamemaliza vifungo vyao ili iwe njia ya kujitengenezea Kipato  baada ya kumaliza vifungo vyao.

Kamishna ametoa rai kwa taasisi nyingine kuhakikisha ziznaanza kutumia Nishati Safi kuendana na agenda ya kitaifa ya Nishati Safi ili kulinda mazingira.

Naye, Mwenyekiti  wa Wanawake na Samia Bi Fatuma Madidi ameipongeza STAMICO  kwa juhudi za kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi na akapigia msumari kwenye suala la kuhakikisha na  taasisi yake hiyo inashiriki kikamilifu kuisambaza Nishati ya Rafiki Briquettes  katika kona zote za Tanzania.

STAMICO  imejipanga  kuhakikisha inaendelea  kuwa kinara katika kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi Tanzania Nzima.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad