HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 25, 2026

IAA KUBORESHA MAZINGIRA YA KUJIFUNZIA ILI KUENDELEA KUZALISHA WATAALAM MAHIRI

 





Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Prof. Eliamani Sedoyeka amesema IAA itaendelea kuimarisha miundombinu na mazingira ya kujifunzia ili kandaa watalaam mahiri na kuendana na mahitaji ya programu za kisasa hususani programu zinazohusisha matumizi makubwa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

Prof. Sedoyeka amesema hayo Agosti 24, 2026 katika hafla ya uzinduzi wa utoaji wa programu za Shahada ya Uhasibu na Teknolojia ya Habari (Bachelor Degree in Accountancy with IT) na Shahada ya Sayansi ya Kompyuta (Bachelor Degree in Computer Science) katika Kampasi ya Babati iliyofanyika Waangw’aray Mjini Babati.

“Tunaishukuru Serikali kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) imetoa jumla ya shilingi bilioni 13.7 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala, mkataba na maabara ya TEHAMA katika Kampasi ya Babati. Sisi pia tumewekeza katika teknolojia na mkakati wetu ni madarasa yetu yote yawe ‘smart classes’ madarasa janja” amesema.

Prof. Sedoyeka ameongeza kuwa dhamira ya IAA ni wanafunzi kujifunza katika mazingira yanayowapa nafasi ya kupata maarifa, kufanya mazoezi, kubuni, kujiandaa kwa mahitaji halisi ya dunia ya kazi na kuwa kutumia maarifa kutatua changamoto halisi.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Daniel Sillo amesema , taasisi za umma na binafsi zinatumia mifumo ya kidijitali katika kusimamia taarifa za fedha, kufanya ukaguzi, kuhifadhi kumbukumbu, kufanya uchambuzi wa taarifa na kutoa maamuzi, hivyo Taifa linahitaji wataalam walioandaliwa vema ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya dunia.

Mbunge wa Babati Mjini, Mhe. Emmanuel Khambay amepongeza Uongozi wa IAA kwa ubunifu huku akieleza umuhimu wa uwepo wa IAA mkoani Manyara kuwa utaongeza fursa za elimu na uchumi kwa Mkoa wa Manyara na mikoa jirani.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo IAA, Dkt. Mwamini Tulli amesema ,”IAA itahakikisha kuwa upanuzi wa huduma za elimu unaendana na ubora wa miundombinu, programu za masomo, teknolojia, rasilimali watu na huduma kwa wanafunzi.”

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad