HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 28, 2026

BAYER YAENDELEZA KAMPENI YA UHAKIKI WA MBEGU MOROGORO

 


KAMPUNI ya Bayer Tanzania imeendelea na kampeni ya kitaifa ya uhamasishaji kwa wakulima, inayolenga kuwahamasisha wakulima wa mahindi kuhakiki mbegu zilizothibitishwa kabla ya kupanda, ili kuongeza tija, kuimarisha usalama wa chakula na kujenga ustahimilivu wa kilimo.


Akizungumza katika kampeni hiyo mkoani Morogoro, Mkurugenzi wa Bayer Tanzania, Sango Mwinyi, amesema wakulima wadogo wanahitaji kupata taarifa sahihi kuhusu mbegu bora na zilizothibitishwa ili kuepuka hasara na kuongeza uzalishaji.


Mwinyi amesema mabadiliko ya tabianchi na hali ya hewa isiyotabirika yanaendelea kuwa changamoto kwa wakulima, hivyo matumizi ya mbegu zilizothibitishwa ni muhimu katika kuongeza tija na ustahimilivu wa kilimo.


Amesema kampeni hiyo inayojulikana kama “DEKALB Mafanikio Shambani” itadumu kwa miezi minne na inalenga kuhamasisha matumizi ya aina tano za mbegu chotara za mahindi za DEKALB, zinazolenga mazingira mbalimbali ya kilimo nchini.


Aidha, Bayer imeanzisha promosheni yenye zawadi mbalimbali kwa wakulima watakaonunua mbegu halisi, ikiwemo pampu za kunyunyizia, simu janja, mashine za kupandia mahindi, pikipiki, mifumo ya umeme wa jua na mashine za kumenya mahindi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad