HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 6, 2026

TUTAIMARISHA UKUSANYAJI WA KODI KWA HAKI NA WELEDI - CG MWENDA

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda, amesema Mamlaka hiyo itaendelea kutekeleza maelekezo ya Rais kuhusu kuimarisha ulipaji wa kodi kwa hiari kwa kuhakikisha kodi inasimamiwa na kukusanywa kwa haki na weledi ili kujenga imani ya walipakodi kwa TRA.

Akizungumza katika kikao cha tathmini ya utendaji kazi wa TRA kwa mwaka wa fedha 2025/2026, Kamishna Mkuu Mwenda amesema katika kikao hicho pia watajadili na kuweka mikakati ya namna ya kutekeleza maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa wakati wa maadhimisho ya miaka 30 ya TRA na utoaji wa Tuzo za Rais Julai Mosi mwaka huu.

Mwenda amesema TRA itaendelea kuwaheshimu walipa kodi wote, huku ikichukua hatua stahiki dhidi ya wanaokwepa kulipa kodi kwa mujibu wa sheria na kuwarudisha kwenye mstari kwa heshima.

Amesisitiza pia kuwa hakutakuwa na "kodi ya dhuluma", akieleza kuwa walipa kodi hawapaswi kuidhulumu nchi kwa kukwepa kodi, na kwa upande mwingine TRA haitawadhulumu walipakodi kupitia makadirio yasiyo sahihi ya kodi.

Aidha, amesema ili kuongeza ulipaji wa kodi kwa hiari ni lazima kujenga imani ya walipa kodi kwa kuhakikisha usimamizi wa kodi wa haki, matumizi yenye uwajibikaji ya mapato ya kodi pamoja na kuboresha huduma zinazotolewa na TRA ili kuwezesha biashara na kurahisisha ulipaji wa kodi.

Mwenda amesema ushirikiano kati ya TRA na walipa kodi umewezesha mafanikio makubwa ya ukusanyaji wa mapato katika kipindi cha miaka 30 ya mamlaka hiyo.

Amebainisha kuwa makusanyo ya kodi yameongezeka kutoka takribani shilingi trilioni 21 kwa mwaka wakati Rais alipoingia madarakani hadi kufikia shilingi trilioni 37.96, sawa na ukuaji wa zaidi ya asilimia 77.















No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad