HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 31, 2026

NMB Foundation, Mercy Corps Washirikiana Kuinua Biashara za E-Mobility

 Taasisi za NMB Foundation na Mercy Corps Tanzania zimesaini makubaliano ya utekelezaji wa mradi wa Evolve wenye thamani ya Shilingi bilioni 2.6 utakaotekelezwa kwa miaka miwili ili kukuza biashara zinazohusiana na usafiri wa vyombo vya moto vinavyotumia umeme jijini Dar es Salaam.

Mradi huo unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya kupitia Enabel unalenga kuwawezesha wanawake, vijana na wafanyabiashara wa E-Mobility kupitia mafunzo ya biashara, ushauri wa kitaalamu pamoja na upatikanaji wa ruzuku na mikopo.

Meneja Mkuu wa NMB Foundation, Nelson Karumuna, alisema awamu ya kwanza itanufaisha zaidi ya biashara 25 huku Mercy Corps ikiongoza utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kuwawezesha wabunifu na wafanyabiashara waliopo katika sekta hiyo.

Washirika wa mradi wanaamini ushirikiano huo utachangia ukuaji wa sekta ya E-Mobility, kuongeza ajira na kuharakisha matumizi ya teknolojia za usafiri safi nchini sambamba na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Meneja Mkuu wa NMB Foundation, Nelson Karumuna (katikati), na Mratibu wa Mercy Corps Tanzania, Anthony Salota, wakionyesha makubaliano ya utekelezaji wa Mradi wa Evolve mara baada ya kusaini MoU jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Virginie Hallet, Mkurugenzi Mkazi wa Enabel Tanzania, na kulia ni Marc Stalmans, Mkuu wa Ushirikiano wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania.

eneja Mkuu wa NMB Foundation, Nelson Karumuna, akipeana mkono na Mratibu wa Mercy Corps Tanzania, Anthony Salota, baada ya kusaini Makubaliano ya Utekelezaji wa Mradi wa Evolve. Kushoto ni Virginie Hallet, Mkurugenzi Mkazi wa Enabel Tanzania, na kulia ni Marc Stalmans, Mkuu wa Ushirikiano wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania.









No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad