HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 11, 2026

Mixx yakabidhi zawadi kwa washindi watatu maonesho ya Sabasaba

 


Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI  ya Mixx imeendelea kuwazawadia wateja wake kupitia kampeni ya Kombe la Dunia ya MiXX Super, ambapo washindi watatu wamekabidhiwa zawadi za shilingi milioni moja kila mmoja kwa kutumia aprication ya MiXX Super app kufanya malipo ya huduma mbalimbali.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi hizo katika banda la Yas kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Meneja wa Biashara Mixx Mkoa wa Dar es Salaam, Estony Venant, alisema kampeni hiyo imeendelea kuwagusa Watanzania wengi huku jumla ya washindi 48 wakinufaika hadi sasa.

Alisema kati ya washindi hao,zaidi ya washindi 20 wamejishindia vifaa mbalimbali kutoka kwa mshirika wa Mixx kampuni ya Hisense, huku washindi wengine zaidi ya 40 wakijishindia fedha taslimu za shilingi milioni moja kila mmoja.

Venant alisema kampeni hiyo bado inaendelea na kwamba mshindi wa mwisho atajishindia zawadi kubwa ya shilingi milioni 50, akiwahimiza wananchi kutumia Aprication ya MiXX Super app katika kufanya malipo ya huduma mbalimbali za kifedha ili kuongeza nafasi ya kushinda.

"MiXX Super ni zaidi ya Aprication malipo; ni jukwaa linalorahisisha huduma za kifedha huku likiwapa watumiaji nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali. Tunawahimiza wananchi kuipakua na kuitumia mara kwa mara," alisema Venant.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad