HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 17, 2026

MiXX Yakabidhi Zawadi kwa Washindi wa Kampeni ya Kombe la Dunia

 Na Mwandishi Wetu

Kampuni ya MiXX imeendelea kuwazawadia wateja wake kupitia kampeni ya "Kombe la Dunia ya Ikiingia Tu... Golii!", inayowapa nafasi ya kujishindia zawadi kwa kufanya malipo ya huduma mbalimbali kupitia MiXX Super App.

Katika wiki ya nane ya kampeni hiyo, washindi sita walitangazwa, ambapo wanne walikabidhiwa fedha taslimu za shilingi milioni moja kila mmoja, huku washindi wawili wakijishindia vifaa vya kisasa vya Hisense.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi hizo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Malipo ya Kidijitali wa MiXX, Mshamma Mshamma, alisema kampeni hiyo imeendelea kuwafikia Watanzania wengi, huku jumla ya washindi 80 wakinufaika tangu ilipoanza.

Alisema washindi wamekuwa wakijishindia fedha taslimu pamoja na vifaa mbalimbali vinavyotolewa kwa ushirikiano na kampuni ya Hisense, jambo linaloonyesha dhamira ya MiXX ya kuwazawadia wateja wake waaminifu.

Mshamma alisema kampeni bado inaendelea, akibainisha kuwa mshindi wa mwisho ataondoka na zawadi kubwa ya shilingi milioni 50.

Aliwahimiza wananchi kuendelea kutumia MiXX Super App kufanya malipo ya huduma mbalimbali za kifedha ili kuongeza nafasi ya kushinda zawadi hizo.

"MiXX Super App ni zaidi ya programu ya malipo. Ni jukwaa linalorahisisha huduma za kifedha huku likiwapa watumiaji nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali," alisema Mshamma.

Mmoja wa washindi, Ibrahim Mandoa, mkazi wa Kinondoni, alisema ushindi wake umempa imani kuwa kampeni hiyo ni ya kweli na inawanufaisha watumiaji wa MiXX Super App.

"Nimefurahi sana kushinda na hii ni mara yangu ya kwanza kupata zawadi kama hii, na ninawahimiza Watanzania kuipakua na kuitumia MiXX Super App mara kwa mara kufanya malipo mbalimbali ili nao wapate nafasi ya kushinda," alisema Mandoa


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad