HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 10, 2026

MBUNGE MARIAM IBRAHIM ACHANGIA MILIONI TANO UJENZI WA SHULE MPYA YA MSINGI KISUTU

Na Mwandishi Wetu, Pwani 

MBUNGE Viti Maalum Mkoa wa Pwani Mariam Ibrahim, amechangia Sh. milioni tano kwa ajili ya ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi Kisutu iliyopo Jimbo la Bagamoyo mkoani humo. 

Ametoa mchango huo wakati aliposhiriki katika  tukio la upandaji wa miti 300 lililofanyika katika eneo la shule hiyo.
Akizungumza na wananchi, Mbunge Mariam amesema mchango huo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa na wananchi pamoja na wadau mbalimbali katika kuhakikisha shule hiyo inakamilika. 

Pia amempongeza Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo CPA Subira  Mgalu, kwa juhudi zake za kusimamia maendeleo ya elimu na kuendelea kushirikiana na wananchi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Aidha, amempongeza  Diwani wa Kata ya Kisutu Awesu Muhidini, kwa uongozi wake na namna anavyoshirikiana na wananchi kuipambania shule hiyo hadi kufikia hatua ya sasa.

Mbunge Mariam pia amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwezesha upatikanaji wa eneo lililojengwa shule hiyo, hatua ambayo imefungua fursa ya kuboresha huduma za elimu kwa watoto wa Kata ya Kisutu.

Katika hafla hiyo,amekabidhi sh. milioni 3 papo hapo, huku akiahidi kuwa Sh. milioni mbili zilizobaki atazikabidhi kupitia Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo CPA Mgalu, ili kukamilisha ahadi yake ya mchango wa Sh.Milioni 5.










 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad