HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 3, 2026

Jeshi la Polisi lahimiza ushirikiano na makampuni ya ulinzi binafsi


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa SGA Tanzania, Oscar Mgaya akizungumza wakati wa hafla hiyo.

Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Ulrich Matei (kushoto) akikabidhi zawadi Kwa John Amon ambaye ni mmoja wa wastaafu wa SGA Tanzania.
Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Ulrich Matei (wa pili kushoto) akisaidiana na wanachama wa Club 20 wa SGA kukata keki wakati wa shughuli ya kuwaaga wafanyakazi waliostaafu na kuwatambua wafanyakazi walihudumia kampuni hiyo kwa zaidi ya miaka 20. 

JESHI la Polisi limetoa wito wa ushirikiano wa karibu kati ya polisi na makampuni binafsi ya ulinzi kwa lengo la kupunguza matukio ya uhalifu pamoja na kudumisha amani nchini.

Wito huo umetolewa hivi karibuni na Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi (DCP) Ulrich Matei wakati wa hafla maalum iliyoandaliwa na kampuni ya ulinzi ya SGA Tanzania iliyolenga kuwaaga watumishi wa kampuni hiyo waliosataafu na kuwatambua wafanyakazi walioitumikia kampuni hiyo Kwa zaidi ya miaka 20.

baada ya kutumikia kampuni hiyo kwa zaidi ya miaka 20 kupitia programu inayojulikana kama Club 20.

Hafla hiyo ilifanyikia katika Bustani ya Hekima jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wawakilishi mbalimbali kutoka Jeshi la Polisi, Baraza la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), uongozi na wafanyakazi wa kampuni ya SGA pamoja na wageni wengine waalikwa.

Alisema kuwa sekta binafsi katika sekta ya ulinzi pia ina jukumu la kuhakikisha nchi inakuwa salama amapo alitoa wito kwa wastaafu walioagwa kuendelea kutoa michango na uzoefu wao ili amani iliyoko hapa nchini iendelee kutamalaki.

DCP Matei aliupongeza uongozi wa SGA kwa kuendelea kuthamini michango inayotolewa na wafanyakazi wake sambamba na kuhakikisha ustawi wa watumishi wa kampuni hiyo ikiwemo kuendelea kuwajengea uwezo.

”Makampuni mengi huwa hayazingatii maagizo yanayoelekeza makampuni binafsi ya ulinzi kuendelea kuwajengea mazingira mazuri ya kiutendaji watumishi wao kupitia mafunzo, uhakiki, usimamizi na maboresho ya mishahara; kwa SGA niwapongeze kwa kujitahidi kutekeleza maagizo haya, nyinyi ni mfano mzuri wa kuigwa na makampuni mengine”, alisema.

Aidha alitoa pongezi kwa uongozi wa kampuni hiyo kwa kuwa na utaratibu wa kuwapongeza wafanyakazi waliofanya kazi kwa zaidi ya miaka 20 na kuongeza kwamba kwa watumishi zaidi ya 95 kufanya kazi kwa zaidi ya miaka 20 ni jambo linalostahili kusherehekewa na kupongezwa.

Alitoa wito kwa makampuni yote ya ulinzi ya binafsi kuongeza ufanisi na kuwekeza zaidi katika teknolojia, mafunzo kwa watumishi wao, kufuata sheria na kuzingatia haki za binadamu ili kupunguza malalamiko wakati wa utoaji wa huduma.

DCP Matei aliahidi kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kutoa ushirikiano wake wa dhati kwa makampuni binafsi jambo ambalo amesema ni muendelezo wa ushirikiano huo kwa miaka mingi iliyopita.

Akizungumza kwa niaba ya SGA Tanzania, Mkuu wa kitengo cha fedha cha kampuni hiyo Bw. Jonathan Geleta, aliushukuru uongozi wa Jeshi la Polisi kwa ushirikiano ambao jeshi hilo limetoa na linaendelea kutoa kwa makampuni binafsi ya ulinzi hapa nchini.

"Nichukue fursa hii kwa niaba ya uongozi wa SGA kuahidi kuwa kampuni yetu itaendelea kufuata miongozo na kanuni zote kama zinavyotolewa na Jeshi la Polisi ili kuhakikisha ufanisi katika kutoa huduma zetu ndani ya jamii”, alisema.

Aliwapongeza wastaafu kwa huduma yao bora waliyotoa wakati wakiitumikia kampuni hiyo, ambapo alitoa rai kwa wastaafu hao kuwa mabalozi wazuri wa kuhimiza amani wakati wakianza maisha mapya ndani ya jamii.

SGA Security ni kampuni ya kwanza ya ulinzi ya kibinafsi nchini Tanzania, iliyoanza kufanya shughuli zake rasmi hapa nchini miaka 42 iliyopita, ambapo kwa sasa inaajiri zaidi ya Watanzania 5,000 katika mtandao wake ulioenea hapa nchini.

Pamoja na huduma nyingine bora, kampuni hiyo pia inatoa huduma bora zaidi ya usafirishaji wa bidhaa zikiwemo zile zenye thamani kubwa kwa usalama wa hali ya juu na uhakika.

SGA pia inatoa huduma za ulinzi wa hali ya juu, huduma za dharura pamoja na vifaa vya usalama wa kielektroniki ambavyo husaidia kuhakikisha usalama wa wateja wake, ambapo kutokana na huduma hizo bora kampuni hiyo imepata tuzo mbalimbali za ndani na nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad