Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MKURUGENZI wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP Centre), , amesema mfumo wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) hauna mbadala ikiwa Tanzania inalenga kufikia uchumi wa thamani ya dola trilioni moja ifikapo mwaka 2050.
Kauli hiyo ameitoa kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X, kufuatia ziara ya Rais wa Singapore, , pamoja na mhadhara wake katika , ambao umeibua mjadala mpana kuhusu safari ya maendeleo ya Singapore kutoka taifa la kipato cha chini hadi kuwa miongoni mwa nchi zilizoendelea zaidi duniani.
Kafulila amesema kuwa kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Fedha Duniani (IMF) za mwaka 2026, Singapore ni miongoni mwa nchi zenye pato kubwa zaidi kwa mtu mmoja mmoja duniani, likifikia zaidi ya dola 107,000 kwa mwaka. Hata hivyo, alibainisha kuwa pamoja na mafanikio hayo makubwa, uchumi wa taifa hilo bado haujafikia dola trilioni moja, ukiwa na thamani ya takribani dola bilioni 659.
Alieleza kuwa mwaka 1995 uchumi wa Singapore ulikuwa karibu sawa na wa Tanzania, ukiwa katika kiwango cha dola bilioni 87, jambo linaloonesha kuwa Tanzania inapaswa kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi kwa kiwango kikubwa zaidi kuliko kilichofikiwa na Singapore ili kutimiza lengo la uchumi wa dola trilioni moja ndani ya kipindi cha miaka 25 ijayo.
“Tunapaswa kubadili namna tunavyofanya kazi, kupanga na kutekeleza miradi ya maendeleo. Hii ndiyo njia pekee ya kufikia malengo makubwa yaliyoainishwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050,” amesema Kafulila.
Ameunga mkono kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, , ambaye amekuwa akisisitiza umuhimu wa mageuzi makubwa katika mifumo ya utekelezaji wa maendeleo ili kufanikisha malengo ya muda mrefu ya taifa.
Wakati huo huo, Rais Tharman Shanmugaratnam amezitaka nchi za Afrika kutumia kikamilifu mfumo wa PPP kwa kuruhusu sekta binafsi kuendesha miradi inayoweza kufanywa kwa ufanisi zaidi, huku serikali zikielekeza nguvu na rasilimali zake katika maendeleo ya watu kupitia elimu, afya na ujuzi.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo, ubora wa rasilimali watu ndio msingi wa ushindani wa taifa katika uchumi wa dunia, akisisitiza kuwa uwekezaji katika watu ndiyo nguzo muhimu ya maendeleo endelevu.
Kauli za viongozi hao zimekuja wakati Tanzania ikiendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuimarisha ushiriki wa sekta binafsi katika miradi ya maendeleo, hatua inayotajwa kuwa muhimu katika kuongeza uwekezaji, ajira na kasi ya ukuaji wa uchumi wa taifa.


No comments:
Post a Comment