

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, , amewataka wanafunzi wa sheria nchini kujenga taaluma zao katika misingi ya nidhamu, ubunifu na uzalendo ili waweze kushindana katika soko la ajira la kimataifa linalozidi kuwa na ushindani.
Ridhiwani alitoa wito huo Juni 5, 2026, alipokuwa akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Kazi na Taaluma ya Shule ya Sheria ya yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Alisema mafanikio katika taaluma za kisasa hayawezi kupatikana bila wataalamu kuzingatia maadili, hususan nidhamu, uzalendo na umahiri wa kitaaluma, mambo ambayo ni muhimu katika kujenga uwezo wa kushindana ndani na nje ya mipaka ya nchi.
“Ni muhimu kwa wanafunzi wa sheria kutambua kuwa dunia ya sasa inahitaji wataalamu wenye uwezo wa kushindana kimataifa huku wakizingatia maadili ya taaluma zao na kulinda maslahi ya taifa lao,” alisema.
Aidha, Ridhiwani alisema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia imeendelea kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya sheria na haki kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma za haki nchini.
Alitaja baadhi ya hatua zilizochukuliwa kuwa ni pamoja na matumizi ya teknolojia katika mfumo wa haki, uwekezaji katika miundombinu ya utoaji haki pamoja na kuhamasisha matumizi ya mifumo mbadala ya utatuzi wa migogoro.
Kwa mujibu wa Ridhiwani, mageuzi hayo yanalenga kuwawezesha wanasheria na watendaji wa vyombo vya haki jinai kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi huku yakichangia kujenga mazingira bora ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Alisisitiza kuwa wataalamu wa sheria wana nafasi muhimu katika kulinda maslahi ya taifa, kuimarisha utawala wa sheria na kuchochea maendeleo endelevu kupitia usimamizi wa haki na sheria.
Maadhimisho hayo yalikusanya wanafunzi, wahadhiri na wadau mbalimbali wa sekta ya sheria kujadili fursa na changamoto zinazokabili taaluma hiyo katika mazingira ya dunia yanayobadilika kwa kasi.

No comments:
Post a Comment