Shigela pia amewataka viongozi wa Geita Gold FC na Manispaa ya Geita kuhakikisha wanafanya usajili wa wachezaji wenye uwezo na ushindani wa hali ya juu ili timu hiyo iweze kuhimili ushindani wa Ligi Kuu na kuwakilisha vyema Mkoa wa Geita.
Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa Geita Gold FC, Zubeir Katwira, amesema mafanikio ya timu hiyo yametokana na ushirikiano mzuri kati ya uongozi wa klabu, Halmashauri ya Manispaa ya Geita, wadhamini na mashabiki waliokuwa bega kwa bega katika kipindi chote cha msimu.
Katwira amesema msaada na mazingira mazuri yaliyowekwa na viongozi yameiwezesha timu kutimiza malengo yake ya kutwaa ubingwa wa Championship na kurejea Ligi Kuu ya NBC.
Geita Gold FC imehitimisha msimu wa Championship ikiwa kileleni mwa msimamo kwa kukusanya pointi 77, na hivyo kutwaa ubingwa wa ligi hiyo pamoja na kufuzu kushiriki Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara katika msimu wa 2026/2027.
Mkuu wa MKOA WA GEITA,Martine Shigela ametoa zawadi ya kiasi cha Shilingi Milioni 40 kwa ajili ya kuipongeza timu hiyo.

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
No comments:
Post a Comment