
Mwakilishi wa PigaBet, Gideon Magana (kushoto), akimkabidhi gari aina ya Toyota IST mshindi wa kampeni ya Shinda Ndinga, Samwel Emmanuel (kulia), ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine Tanzania (SAUT), jijini Mwanza. Samwel amesema gari hilo litamsaidia kumalizia masomo yake, kuanzisha shughuli za kujiongezea kipato, pamoja na kuisaidia familia yake.
Samwel Emmanuel akifurahia gari lake aina ya Toyota IST baada ya kukabidhiwa rasmi na PigaBet jijini Mwanza kupitia kampeni ya Shinda Ndinga.
Gideon Magana, mwakilishi wa PigaBet (kushoto) akimkabidhi Samwel Emmanuel, mwanafunzi wa SAUT Mwanza, nyaraka za gari aina ya Toyota IST aliloshinda kupitia kampeni ya Shinda Ndinga ya PigaBet, jijini Mwanza.
Na Mwandishi Wetu.
●Samwel Emmanuel asema gari hilo litamsaidia kumalizia masomo, kuanzisha kipato na kusaidia familia
Mwanza, Tanzania, 26 Juni 2026 – PigaBet imemkabidhi Samwel Emmanuel, mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha SAUT Mwanza, gari aina ya Toyota IST aliloshinda kupitia kampeni ya Shinda Ndinga.
Makabidhiano hayo yamefanyika jijini Mwanza, ambako Samwel anaishi na kusoma. Kabla ya kukabidhiwa gari hilo, Samwel alisafiri kwa ndege kwa mara ya kwanza kwenda Dar es Salaam kukamilisha taratibu za nyaraka za umiliki.
Samwel, mwenye umri wa miaka 24, ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu anayesomea Procurement, Logistics and Supply Chain Management katika SAUT Mwanza. Ametokea Wilaya ya Busega mkoani Simiyu.
Kwa mujibu wa Samwel, taarifa za ushindi wake zilipokelewa kwa mshangao mkubwa na familia yake pamoja na marafiki zake, kwa kuwa hawakuamini mara moja kuwa ameshinda gari kupitia kampeni hiyo.
“Nilipopigiwa simu, nyumbani hawakuamini,” alisema Samwel. “Baada ya kuthibitisha taarifa, furaha ilikuwa kubwa sana.”
Samwel alisema mama yake na bibi yake walikuwa wakimpigia simu mara kwa mara kufuatilia safari yake na kuhakikisha kila hatua inaenda vizuri.
“Bibi na mama hawakulala. Walikuwa wananipigia simu kila mara kujua kama kweli naenda kuchukua gari,” alisema.
Akizungumzia ushindi huo, Samwel alisema gari hilo ni mwanzo wa hatua mpya katika maisha yake, hasa baada ya kumalizia miezi miwili iliyobaki katika masomo yake.
“Najisikia furaha kubwa sana. Siwezi kuelezea furaha niliyonayo. Namshukuru Mungu,” alisema Samwel. “Nitamalizia masomo yangu, kisha gari nitalitumia kwa biashara. Nataka linisaidie mimi na familia yangu.”
Samwel alisema mpango wake ni kulitumia gari hilo kwenye biashara ya taxi kwa kuajiri dereva ili liweze kumuingizia kipato. Pia ana ndoto ya kuwekeza kwenye kilimo na biashara ya mazao, ikiwemo mahindi na mpunga.
Arthur Kazola, Meneja Masoko wa PigaBet, alisema kampeni ya Shinda Ndinga ni sehemu ya juhudi za kampuni kuwashirikisha na kuwazawadia wateja wake.
“Tunampongeza Samwel Emmanuel kwa ushindi huu. Simulizi yake imeonesha namna kampeni hii ilivyogusa maisha ya mshindi na familia yake. Kwetu, hii siyo tu makabidhiano ya gari; ni furaha ya mshindi, familia yake na jamii inayomzunguka,” alisema Kazola.
PigaBet ilimpongeza Samwel na kuwashukuru wateja wote walioshiriki kampeni ya Shinda Ndinga.



No comments:
Post a Comment