Hapi ameyasema hayo wakati akizungumza na wanachama wa Jumuiya ya Wazazi katika ukumbi wa CCM wilayani Bukombe mkoani Geita, akiwa katika ziara yake ya kichama ya kuimarisha shughuli za jumuiya hiyo.
Hapi ameeleza kuwa jumuiya hizo zikiendelea kusikiliza na kutatua kero za wananchi, hususan vijana, chama kitaendelea kupata nguvu na kuaminiwa zaidi na jamii kutokana na mchango wake katika kutatua changamoto mbalimbali za kijamii na kiuchumi.
Kwa upande wake, Naibu Waziri Mkuu Mstaafu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Doto Biteko, amesema maendeleo ya taifa yanategemea uwepo wa watoto wanaolelewa katika maadili mema na kuandaliwa kuwa wazalendo wenye bidii katika uzalishaji mali.
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Geita, Lucas Mazinzi, amesema hali ya kisiasa wilayani Bukombe inaendelea kuwa tulivu kutokana na utekelezaji wa shughuli mbalimbali za chama, ikiwemo ziara za viongozi katika mashina ya CCM na usimamizi wa miradi ya maendeleo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Paskasi Muragili, amesema hali ya ulinzi na usalama wilayani humo ni nzuri na inaendelea kuimarika. Amebainisha kuwa mafanikio katika sekta ya elimu yameongezeka, ambapo idadi ya shule za msingi imeongezeka kutoka 80 mwaka 2021 hadi 100 kwa sasa, huku shule za sekondari zikiongezeka kutoka 16 hadi 30 katika kipindi hicho.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Ally Hapi, anatarajiwa kuhitimisha ziara yake mkoani Geita leo, baada ya kuanza ziara hiyo tarehe 15 mwezi huu kwa lengo la kuimarisha shughuli za chama na jumuiya zake katika mkoa huo.



.jpeg)


No comments:
Post a Comment