HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 5, 2026

Finland na Tanzania waimarisha ubia wa misitu kupitia jukwaa la biashara na uwekezaji

 


UBALOZI wa Finland nchini Tanzania, kwa ushirikiano na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania kupitia Mpango wa Ubunifu wa FUNGUO, wameadhimisha Siku ya Misitu ya Finland 2026 yenye kaulimbiu “Kufanya Biashara na Finland.”

Tukio hilo limewakutanisha wafanyabiashara, wawekezaji, taasisi za Serikali, wadau wa maendeleo, wajasiriamali, na wataalamu wa misitu kutoka Finland na Tanzania ili kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na ukuaji endelevu katika sekta ya misitu.

Mpango huu ulihusisha mada kuu kuhusu fursa za uwekezaji katika sekta ya misitu Tanzania, mawasilisho kutoka kwa makampuni ya Finland, jukwaa maalumu la kukutanisha , na maonyesho ya ufumbuzi endelevu wa misitu kutoka nchi zote mbili.

Hafla hii pia ilishuhudia uzinduzi wa muongozo maalumu wa uwekezaji katika sekta ya misitu (Tanzania Forest Sector Investment Guide).

Akizungumza juu ya umuhimu wa tukio hilo, Balozi wa Finland Tanzania Theresa Zitting amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kibiashara wa nchi hizi mbili. “Ushirikiano madhubuti wa kibiashara ni muhimu katika kufungua fursa zote za sekta ya misitu Tanzania. Siku ya Misitu ya Finland inatoa fursa ya kipekee kwa makampuni, wabunifu, na wawekezaji kutoka nchi zote mbili kujenga uhusiano, kubadilishana ujuzi, na kubainifursa za kivitendo za ushirikiano,” alisema Balozi Zitting na kuongeza kuwa tukio hili linaashiria dhamira ya muda mrefu ya Finland katika maendeleo endelevu ya kiuchumi ya Tanzania kupitia uwekezaji, ubunifu, na ushirikiano na sekta binafsi.

Akiwakilisha Serikali ya Tanzania Mkurugenzi wa Misitu na Ufugaji wa Nyuki, Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Daniel Pancras, ameupongeza mpango huu na kusisitiza jinsi unavyoendana na vipaumbele vya maendeleo vya Tanzania. “Sekta ya misitu ya Tanzania ina fursa nyingi kubwa ambazo bado hazijatumiwa kikamilifu, na Finland imekuwa miongoni mwa wabia wetu thabiti na wenye mchango mkubwa katika kufanikishahili. Uhusiano wa namna hii wa kibiashara wa moja kwa moja ndio hasaunaohitajika ilikutafsiri malengo yetu ya pamoja kuwa ajira, kuongeza thamani, na ukuaji endelevu.”

Taasisi ya Finnpartnership imewasilisha huduma zake kwa washiriki wa Tanzania, ikitengeneza fursa mpya za ushirikiano na makampuni ya Finland na upatikanaji wa mifumo ya ufadhili wa pamoja iliyoundwa kusaidia ukuaji wa biashara na ubia wa kimataifa.

Akizungumza kwaniaba ya FinFund, Naibu AfisaMtendaji Mkuu Minnamari Marttila ameangazia fursa za mageuzi zinazotokana na mikutano ya kibiashara iliyoratibiwa vizuri. “Siku ya Misitu ya Finland inatengeneza mazingira, ambapo makampuni yanaweza kwenda mbalizaidi ya utambulisho tu na kuanza kujenga uhusiano wa maana wa kibiashara kupitia kubadilishana ujuzi, uhamishaji wa teknolojia, uwekezaji, na ushirikiano wa mudamrefu wa kibiashara.”

Kivutio kikuu cha siku hii kimekuwa ni maonyesho ya makampuni yanayofadhiliwa kupitia Mpango wa #GreenCatalyst, ambao unaofadhiliwa na Finland chini ya Mradi wa Ubunifu wa FUNGUO unaomilikiwa na UNDP Tanzania. Mpango huu unakamilisha mradi mkubwa zaidi wa Finland unaojulikana kama FORLAND wenye thamani ya Sh61 bilioni za Kitanzania, ukiimarisha zaidi usaidizi wa ukuaji endelevu na jumuishi katika sekta ya misitu Tanzania.

Kupitia awamu yake ya kwanza ya ufadhili, Mpango wa #GreenCatalyst umewekeza zaidi ya Sh1 bilioni za Kitanzania katika makampuni 14 yanayoendeleza misitu endelevu, usindikaji wa mbao unaoongeza thamani, teknolojiazinazohimili mabadiliko ya tabianchi, na ufumbuzi wa uchumi mzunguko.

Uwekezaji huu unajengwa juu ya dhamira ya muda mrefu ya Finland katika sekta ya misitu Tanzania. Ndani ya kipindi cha miakakumi (10), Finland imewekeza €45 milioni (takribani Sh136.3 bilioni za Kitanzania) katika sekta hii, ikisaidia usimamizi endelevu wa misitu, uendelezaji wa ujuzi, ubunifu, na ushirikiano wa sekta binafsi unaochangia ukuaji wa uchumi na uendelevu wa mazingira.

Akizungumza kwa niaba ya UNDP Tanzania, Meneja wa Mradi wa FUNGUO Joseph Manirakiza aliangazia nafasi ya ushirikiano katika kukuza ubunifu. “Ubunifu unastawi pale ambapo wajasiriamali wanapatasiotu ufadhili, bali pia mitandao, masoko, na ushirikiano. Siku ya Misitu ya Finland ni jukwaa la aina yake ambalo wajasiriamali wetu wa #GreenCatalyst wanalihitaji ili kuunganishwa na kukua,” alisema Manirakiza.

Naye mwakililishi wa FORLAND ambao ni mradi unaojihusisha na misitu, matumizi sahihi ya ardhi na kuongeza thamani katika mazao ya misitu, Bw. Masasa Makwassa aliipongeza Finland kw akuadhimisha siku hii muhimu na kusisitiza kuwa shirika hilo litaendelea kushirikiana na wadau wote kuhakikisha malengo ya mradi huo unotekelezwa kwa pamoja na Tanzania na Finland yanafikiwa.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad