HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 9, 2026

BENKI YA NMB YATANGAZA AWAMU MPYA YA UKUAJI BAADA YA MUDA WA KATI WA MWAKA 2021/2025 KUREKODI FAIDA

Benki ya NMB imetangaza kuingia katika awamu mpya ya ukuaji baada ya kukamilisha Mpango wake wa Muda wa Kati wa mwaka 2021 hadi 2025, uliowezesha benki hiyo kurekodi faida kabla ya kodi ya zaidi ya Sh1 trilioni na kuongeza mchango wake katika uchumi wa Tanzania.

Akizungumza wakati wa mkutano wa wawekezaji jijini Dar es Salaam kuelekea Mkutano Mkuu wa 26 wa Wanahisa, Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, alisema miaka mitano iliyopita imejenga taasisi imara zaidi, yenye mtindo wa biashara wenye ustahimilivu na msingi thabiti wa kuingia katika awamu inayofuata ya ukuaji.

Katika kipindi hicho, NMB ilieleza kuwa imeelekeza zaidi ya Sh28 trilioni katika sekta za kimkakati na jumuishi, kwa miaka minne (2021- 2024) imelipa zaidi ya Sh700 bilioni kama gawio kwa wanahisa ( imechangia Sh2.7 trilioni katika kodi na kuwekeza Sh24 bilioni katika miradi ya maendeleo ya jamii.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, alisema taasisi kama NMB zina nafasi muhimu katika kukuza uchumi rasmi, kupanua upatikanaji wa mitaji na kuunga mkono utekelezaji wa Dira 2050, huku NMB ikisema awamu yake ya sasa (Agenda 2030 inalenga zaidi ufadhili endelevu, huduma za kidijitali, huduma bora zaidi kwa wateja na fursa za ukuaji wa kikanda.

Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, akisalimiana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, wakati wa mkutano wa wawekezaji uliofanyika jijini Dar es Salaam kuelekea Mkutano Mkuu wa 26 wa Wanahisa wa benki hiyo.


Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, akizungumza wakati wa mkutano wa wawekezaji uliofanyika jijini Dar es Salaam kuelekea Mkutano Mkuu wa 26 wa Wanahisa wa benki hiyo.



Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, akizungumza wakati wa mkutano wa wawekezaji uliofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo benki hiyo iliwasilisha mafanikio ya Mpango wake wa Muda wa Kati wa mwaka 2021 hadi 2025 na mwelekeo wake wa awamu inayofuata ya ukuaji unaoendana na ajenda ya maendeleo ya Tanzania. Kutoka kushoto ni Afisa Mkuu wa Fedha, Juma Kimori; Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NMB, David Nchimbi, wa pili kulia; na Mkurugenzi wa Uhusiano na Wawekezaji, Uendelevu na Mawasiliano, Innocent Yonazi. (kulia)








No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad