Meneja wa Huduma za Jamii na Matuko wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kutoka kushoto), akikabidhi vifaa vya hospitali kwa Muuguzi Kiongozi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja, Bi. Shufaa Kaniki (kulia), katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Makamu wa Rais wa The Runners Club, Bw. Godfrey Mwangungulu, pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa hospitali. Utoaji huu wa vifaa, wenye lengo la kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto, umefuatia mafanikio ya mbio za Absa Dar City Marathon zilizofanyika tarehe 3 Mei 2026 jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja wakionesha vifaa vipya vya hospitali walivyokabidhiwa na Meneja Huduma za Jamii na Matukio wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (kushoto), katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Utoaji huu, wenye dhamira ya kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto, umewezekana kufuatia mafanikio ya mbio za Absa Dar City Marathon zilizofanyika tarehe 3 Mei 2026, jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa The Runners Club, Bw. Godfrey Mwangungulu, akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa vya hospitali vilivyotolewa na Benki ya Absa Tanzania jijini Dar es Salaam jana. Mchango huu Kutoka Benki ya Absa, wenye lengo la kuunga mkono huduma za afya ya mama na mtoto, umewezekana kufuatia mafanikio ya mbio za Absa Dar City Marathon zilizofanyika tarehe 3 Mei 2026 jijini Dar es Salaam.
Muuguzi Kiongozi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja, Bi. Shufaa Kaniki, akitoa shukrani zake baada ya kupokea msaada wa vifaa vya hospitali kutoka kwa Meneja Huduma za Jamii na Matukio wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (kushoto), katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Utoaji huu, unaolenga kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto, umefuatia mafanikio ya mbio za Absa Dar City Marathon zilizofanyika tarehe 3 Mei 2026 jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment