Na Mwandishi Wetu
WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameshiriki katika semina kuhusu Mpango Mkakati wa Gridi ya Maji ya Taifa.
Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa Bunge wa Msekwa,Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri katika mada yake amesema Gridi ya Maji ya Taifa ni mfumo wa kimkakati wa usambazaji maji kutoka kwenye vyanzo vya uhakika na kuyapeleka katika maeneo yenye uhaba wa maji nchini.
Ameongeza hadi sasa Wizara ya Maji imekamilisha vipande vya mtandao wa Taifa wa maji ikiwamo kutoa maji ziwa Victoria kwenda mikoa ya Shinyanga, Tabora na Shelui katika mkoa wa Singida.
Kwa upande wake Waziri wa Maji Jumaa Aweso akihitimisha mada amewaomba ushirikishwaji wa jamii na ushirikiano kwa wabunge wote ili kuhakikisha mpango mkakati wa Gridi ya Maji ya Taifa unafanikiwa ili kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma ya majisafi na salama na kuchochea ukuaji wa uchumi ili kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo (DIRA 2050)..jpeg)
.jpeg)


.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

No comments:
Post a Comment