Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amehitimisha mgogoro wa nyumba uliopo eneo la mikocheni kiwanja namba 317 Regent Estate ambapo amesema kuwa kwa mujibu wa nyaraka zilizopo nyumba hiyo ni mali ya Godifrey Shuma na Carista Shuma, na amemtaka Bi Everlin Chiomba aliyekuwa akiishi hapo akidai nyumba hiyo ni mali yake aliyorithi kutoka kwa marehemu mumewe kuondoka kwenye nyumba hiyo ndani ya muda wa saa moja na nusu
Akizungumza katika mtaa wa Rigent eneo la Mikocheni wilaya ya Kinondoni jijini Dar e Salaam Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila amesema Godifrey Shuma na Carista Shuma ndio wamiliki halali wa nyumba hiyo kwa mujinu wa maelekezo ya mahakama na kwa mujibu wa nyaraka zilizopo, hivyo amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na RPC wa Kinondoni kusimamia zoezi hilo ili mwenye haki akabidhiwe huku akimtaka Bi Everlin Chiomba kurejea Mahakamani endapo atakuwa hajaridhika na maamuzi hayo .
RC Chalamila ameongeza kuwa yupo tayari kumsaidia Bi Everlin Chiomba kirejea mahakamani kupata ufafanuzi zaidi na ushauri wa kitaalamu lakini kwa nyaraka zilizopo mmiliki halali ni Godifrey Shuma na Carista Shuma pia ameitaka ofisi ya Ardhi na mahakama kumsaidia kumaliza kitendawili cha binti aliejitokeza hapo akidai ni mtoto wa marehem Chiomba aliekuwa mmiliki wa nyumba hiyo wa awali kwani mtoto huyo anaomekana ana majina mawili tofauti ambayo ni Flora Chiomba na Flora Mwashaa
Aidha kabla ya uamuzi huo hapo awali Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam aliunda kamati ya kufuatilia suala hilo ambapo Mwenyekiti wa kamati hiyo ya mgogoro Mbaraka Forogo alipotoa taarifa ya kamati amesema kamati imejiridhisha kuwa nyumba hiyo ni kweli iliuzwa na kwamba Godifrey Shuma ndiyo mwenye hati miliki ya nyumba hiyo kwa sasa
Vilevile kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule amekemea kitendo klichofanywa na mtoto anayedai ni wa marehemu Chiomba Bi Flora kileta Mabaunsa kufanya fujo wakati walishapiga marufuku kutumia mabaunsa pia Kamishina msaidizi wa ardhi Mkoa wa Dar es salaam Bw Shukrani Kyando akieleza kuwa Godifrey Shuma na Carista Shuma ndiyo wamiliki halali kwa mujibu wa nyaraka.
Awali pande zote mbili za wadai zilipewa fursa ya kujieleza juu ya sakata hilo huku pande zote mbili zikieleza kuwa wao ndio wamiliki


.jpeg)


No comments:
Post a Comment