Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ameongoza zoezi la utoaji wa Tuzo za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) zilizotolewa kwa wanamichezo na timu zilizofanya vizuri mwaka 2025, katika hafla iliyolenga kutambua mchango na mafanikio ya wadau wa michezo nchini.
Akizungumza katika hafla hiyo ambapo alikuwa mgeni rasmi, Dkt. Nchemba alitoa pongezi na shukrani za dhati kwa Ecobank Tanzania kwa mchango wake mkubwa wa kudhamini hafla hiyo muhimu ya michezo nchini.
Dkt. Nchemba alisema ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi unaendelea kuwa chachu ya maendeleo ya michezo nchini, huku akiipongeza Ecobank Tanzania kwa kuonyesha dhamira ya kweli katika kuunga mkono vipaji vya wanamichezo wa Tanzania. Alibainisha kuwa udhamini huo umeongeza hadhi ya Tuzo hizo na kutoa motisha kwa wanamichezo kuendelea kufanya vizuri katika mashindano ya kitaifa na kimataifa.
Aidha, Waziri Mkuu alisema katika kipindi kifupi yameshuhudiwa mafanikio makubwa katika sekta ya michezo, yakiwamo kuanzishwa kwa Mfuko wa Maendeleo ya Michezo unaopata asilimia tano ya mapato ya michezo ya kubashiri, hatua ambayo imewezesha timu na wanamichezo kushiriki mashindano mengi zaidi kwa ubora wa hali ya juu. Alisisitiza kuwa mchango wa wadau kama Ecobank Tanzania unaendelea kusaidia juhudi za Serikali katika kuinua sekta ya michezo na kuibua vipaji vya vijana nchini.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Dkt. Charles Asiedu alisema benki hiyo inajivunia kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutambua na kuinua vipaji vya michezo mbalimbali hapa nchini kupitia Tuzo za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) tukio linaloadhimisha ubora, kujituma na mafanikio makubwa ya mashujaa wa michezo wa Tanzania.
Dkt. Asiedu alisema kupitia Tuzo hizo maalumu, Ecobank imedhamini kipengele cha Tuzo ya Mwamuzi Bora wa Kiume wa Mwaka, kinacholenga kutambua na kuhamasisha vipaji vinavyochipukia katika sekta ya michezo nchini. Alieleza kuwa benki hiyo itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha vijana wenye vipaji wanapata motisha na mazingira bora ya kufikia mafanikio yao.
" Ecobank Group ni benki kubwa yenye mtandao mpana zaidi barani Afrika, ikiwa na uwepo katika nchi zaidi ya 33. Nchini Tanzania, Ecobank inatoa huduma mbalimbali za kibenki kwa wateja binafsi pamoja na wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa." Alisema Dkt. Asiedu
Benki hiyo imeendelea kuwakaribisha wananchi kutumia huduma zake kupitia matawi, mawakala pamoja na ATM zilizopo Dar es Salaam, Arusha na Mwanza ili kupata huduma bora na za kisasa za kibenki. Sambamba na hilo, Ecobank pia inatoa huduma za kibenki kiganjani kupitia Ecobank Mobile, ambapo wateja wanaweza kupata huduma mbalimbali ikiwamo kufungua akaunti, kulipia bili, kupata huduma ya salary advance kwa waajiriwa pamoja na mikopo kwa watumishi wa umma.
Kwa pamoja, Serikali na wadau wa sekta binafsi wanaendelea kuibua vipaji, kuhamasisha jamii na kuwezesha kizazi kijacho kupitia michezo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akizungumza na viongozi pamoja na wageni mbalimbali wakati wa utoaji wa Tuzo za BMT 2025 zililizofanyika katika ukumbi wa The Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Dkt. Charles Asiedu akimtangaza mshindi Tuzo ya Mwamuzi Bora wa Kiume wa Mwaka katika Tuzo za BMT 2025 zilizotolewa katika ukumbi wa The Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Dkt. Charles Asiedu(kulia) akimkabidhi Tuzo ya Mwamuzi Bora wa Kiume wa Mwaka, Shabani Mahobonya (kushoto) kwenye Tuzo za BMT 2025 zilizotolewa katika ukumbi wa The Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam
Wafanyakazi wa Ecobank Tanzania wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Dkt. Charles Asiedu(wa kwanza kushoto) wakiwa kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo za BMT 2025.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba pamoja na viongozi wengine wakiwa kwenye picha ya pamoja na wadhamini wa Tuzo za BMT 2025.
Wafanyakazi wa Ecobank Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja katika Tuzo za BMT 2025







No comments:
Post a Comment