*************
Tabasamu la kujiamini linaonekana usoni mwa Sifael Mboma (15), mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Songwe iliyopo wilayani Momba mkoani Songwe. Licha ya kusoma katika shule iliyoko pembezoni mwa mji, ana ndoto kubwa ya kuwa mhandisi siku moja.
Kwa Sifael, sayansi siyo tu masomo ya darasani bali ni sehemu ya maisha ya kila siku. Anazungumzia masomo ya sayansi kwa msisimko na kujiamini akieleza namna yanavyomvutia na kumpa mwelekeo wa maisha yake ya baadaye.
“Ukiangalia maisha yetu ya kila siku yamezungukwa na sayansi kama vile uhandisi. Tunaishi katika nyumba na majengo yaliyojengwa kwa utaalamu huo,” anasema kwa msisitizo.
Anapozungumzia masomo ya sayansi, macho yake yanang’aa na uso unakuwa na nuru zaidi ishara ya kumaanisha anachokiamini. Anaeleza kuwa, majaribio ya vitendo katika maabara hasa kwenye somo la kemia humjengea hamasa ya kujifunza. Anasema, kuchanganya asidi na besi na kushuhudia matokeo yake papo kwa hapo kwake siyo tu jaribio, ni uzoefu unaochochea bidii kuifikia ndoto yake.
Sifael anasema, sayansi ni daraja la suluhu za changamoto katika jamii. Anaamini kuwa kujikita katika taaluma hizo kutasaidia kuongeza idadi ya wataalamu wa kike katika sekta muhimu kama uhandisi na udaktari.
“Wanawake wanapopata huduma kutoka kwa wataalamu wenzao, wanakuwa huru na kupata faraja zaidi,” anasema.
Sifael pia ana ujumbe mzito kwa wasichana wenzake kuwa waachane na hofu na dhana potofu kwamba masomo ya sayansi ni magumu au ni ya wavulana pekee.
Hadithi ya Sifael si ya kipekee bali ni sehemu ya wimbi jipya la wasichana mkoani Songwe wanaoanza kuonyesha uthubutu katika masomo ya sayansi.
Katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Songwe, mafanikio yanaonekana wazi. Mkuu wa shule hiyo Bi. Janeth Mwamwile anasema kati ya wanafunzi 25 waliohitimu kidato cha nne mwaka 2025, 12 walipata daraja la kwanza, wanne daraja la pili, wanane daraja la tatu, mmoja daraja la nne na hakuna aliyepata daraja sifuri ishara ya mabadiliko chanya yanayochipuka.
Katika wilaya jirani ya Mbozi, simulizi kama hiyo inaendelea kujitokeza. Judith Mgode mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Ndugu na Edna Rajab wa kidato cha tatu kutoka Shule ya Sekondari Shiwinga, ni miongoni mwa wasichana wanaothibitisha kuwa uwezo wa kufaulu masomo ya sayansi hauchagui jinsia. Judith anasisitiza kuwa mafanikio yanahitaji bidii na nidhamu, bila kujali somo analosoma mwanafunzi.
Mabadiliko haya yanaungwa mkono na takwimu ambapo katika Shule ya Sekondari Ndugu Mkuu wa shule hiyo Bw. Cosmas Nzowa anasema, kwa sasa wasichana wanaongoza katika mkondo wa sayansi. Kati ya wanafunzi 158 wanaosoma masomo ya sayansi, 100 ni wasichana sawa na asilimia 63.2.
Nzowa anahusisha mafanikio hayo na maboresho ya mazingira ya kujifunzia hususan ukarabati wa maabara tatu za sayansi kupitia ushirikiano wa UNICEF na Mfuko wa Elimu wa Taifa unaosimamiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).
“Mwaka jana tulikuwa na wanafunzi 70 wa sayansi, lakini mwaka huu wameongezeka na wamefikia 158 baada ya kukamilika kwa maabara hizi,” anasema.
Katika Shule ya Sekondari Shiwinga, hali ya ujifunzaji wa masomo ya sayansi imebadilika kwa kiasi kikubwa. Mwalimu wa sayansi Bw. Remmy Manfred Mwakifuna anaeleza kuwa awali walikuwa na maabara moja ndogo iliyoweza kuhudumia wanafunzi wachache, hali iliyowalazimu kufanya baadhi ya majaribio darasani. Kupitia ukarabati huu wa maabara mbili kwenye shule yetu, wanafunzi wanapata fursa ya kujifunza kwa vitendo katika mazingira bora zaidi anasema Bw. Mwakifuna.
Nae Kaimu Mkuu wa shule hiyo Bw. Ibrahim Nelson Mgalle anasema, anaamini maboresho hayo yataongeza ufaulu wa wanafunzi huku akitoa shukrani kwa Serikali pamoja na wadau wa maendeleo waliofanikisha juhudi hizo za kukamilika kwa maabara za sayansi.
Kwa ujumla, simulizi ya wasichana wa Songwe inaonyesha wazi kuwa mipaka ya kijinsia katika elimu ya sayansi inaanza kuvunjwa. Ndani ya maabara hizo si kemikali pekee zinazochanganyika ama kufanyiwa majaribio, bali pia ndoto, juhudi na matumaini ya kizazi kipya cha wanawake wataalamu kinatengenezwa na kuandaliwa.

Mwalimu wa masomo ya Sayansi Shule ya Sekondari Shiwinga ya Wilayani Mbozi, Songwe Bw. Remmy Mwakifuna akiwa na wanafunzi kwenye moja ya maabara ya Sayansi iliyofanyiwa ukarabati kwa ufadhili wa UNICEF ikishirikiana na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).
▪ Hamasa ya maabara na ari ya wanafunzi vyavunja dhana potofu, wasichana waibuka vinara wa masomo ya sayansi.

Wanafunzi wakifanya mafunzo kwa vitendo ndani ya maabara ya kisasa shule ya Sekondari Ndugu iliyopo Mkoani Songwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi.
Mwanafunzi Sifael Mbona wa kidato cha tatu Shule ya Sekondari ya Wasichana Songwe iliyopo Wilayani Momba mkoani Songwe, akiongea mbele ya shule yao jinsi gani wanafurahia miundombinu mizuri na bora iliyofadhiliwa na UNICEF kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) shuleni kwao.
Muonekano wa matundu nane ya vyoo ya kisasa yaliyojengwa na UNICEF ikishirikia na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), katika Shule ya Sekondari ya wasichana Songwe iliyopo Wilayani Momba mkoani Songwe kwa lengo la kuboresha mazingira ya kujifunzia shuleni hapo.

Muonekano wa maabara ya kisasa iliyokarabatiwa kwa ufadhili wa UNICEF ikishirikana na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA, Shule ya Sekondari Ndugu iliyopo Wilayani Mbozi mkoani Songwe.

No comments:
Post a Comment