Na Mwandishi Wetu
WADAU wote wa Tiba Asili, Afya na Mazingira nchini Tanzania wameshauriwa kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali, mashirika na jamii katika uhifadhi wa mazingira Barani Afrika pamoja na kuunganisha nguvu katika kulinda rasilimali za asili na kuendeleza tiba asili kama utambulisho wa bara na dunia kwa ujumla.
Hayo yamesemwa leo Aprili 18,2026 wakati wadau wa Tiba Asili, Afya na Mazingira nchini, Afrika na Duniani kwa Ujumla wamepata fursa ya kujifunza kutoka katika maisha na mchango wa mwanamazingira mashuhuri duniani, David Attenborough, aliyezaliwa Aprili 18,1926.
Kwa mujibu wa wadau yao kupitia kazi yake David Attenborough ameonesha kwa vitendo umuhimu wa kulinda mazingira, kuheshimu viumbe hai na kuthamini rasilimali za asili kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kukumbuka kuzaliwa kwa mwanamazingira huyo, Katibu Mkuu
Shirika la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira (TRAMEPRO) Boniventura Mwalongo amesema amesisitiza umuhimu wa kıla mmoja wetu wakiwemo wadau kuwa mabalozi wa uhifadhi wa mazingira na matumizi sahihi ya rasilimali
huku kwa viongozi kusimamia sera na sheria zinazolinda mazingira na afya ya jamii
Pia amesisitiza umuhimu wa kushirikiana katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi na uharibifu wa bioanuwai huku akitoa rai kwa waandishi wa habari kuelimisha umma kuhusu uhusiano kati ya mazingira, afya na maendeleo jamii kwa ujumla:
Kuhusu maisha ya David Attenborough amesema wanapaswa kujifunza kutoka katika maisha ya mwanamazingira huyo kwa kuchukua hatua madhubuti sambamba na kuimarisha mshikamano wa kitaifa na kimataifa.“Kulinda mazingira ni kulinda afya, uchumi na maisha ya dunia.”
Akifafanua zaidi amesema kupitia kazi yake, ameonesha kwa vitendo umuhimu wa kulinda mazingira, kuheshimu viumbe hai na kuthamini rasilimali za asili kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
“Katika dunia ya sasa inayokabiliwa na changamoto za mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa misitu na kupungua kwa bioanuwai, ujumbe wake unatukumbusha kuwa hatua za haraka na za pamoja zinahitajika ili kulinda mustakabali wa dunia yetu.”
Aidha amesema katika muktadha wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025–2050, nchini Tanzania uhifadhi wa mazingira ni msingi muhimu wa maendeleo ya uchumi, afya na ustawi wa jamii.
Amefafanua dira hiyo inalenga Tanzania yenye uchumi imara unaotegemea matumizi endelevu ya rasilimali, jamii yenye afya bora na ustawi wa kudumu, usimamizi madhubuti wa mazingira na bioanuwai
“Hivyo basi, kulinda mazingira ni wajibu wa kila mdau kuanzia ngazi ya familia hadi kimataifa.
Kuimarisha Vyanzo vya Dawa kwa Uendelevu

.jpeg)

No comments:
Post a Comment