NI Jumatano nyingine tena ya kushuhudia wababe wa Ulaya wakikiwasha kuitafuta Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa. Huku Arsenal Kule Sporting CP, Je nani kusonga mbele?
Arsenal atamleta Emirates Sporting CP kwenye mechi ya marudiano huku hii ikiwa ni mechi yenye presha kwelikweli kwani kila timu inataka kwenda Nusu Fainali ya michuano. Lakini The Gunners wanaingia uwanjwani wakiwa na faida ya goli 1.
Matokeo hayo yamewapa faida muhimu ya kisaikolojia na kiufundi, lakini bado hawajamaliza kazi, kwani Sporting CP wana uwezo wa kubadili mwelekeo wa tai hii ikiwa Arsenal hawatakuwa makini nyumbani kwani hata hivyo takwimu za mechi ya kwanza wenyeji hawakuwa vibaya sana.
Ushindi wa ugenini wa Arsenal unamaanisha kuwa wanaweza kucheza kwa utulivu zaidi, lakini hilo pia linaweza kuwa hatari kama wataamua kujilinda kupita kiasi. Chini ya kocha Mikel Arteta, Arsenal wamekuwa timu inayopenda kumiliki mpira na kudhibiti tempo ya mchezo.
Cheza michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao ujishindie pesa nyingi hapa. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Hata hivyo, tatizo lao kubwa bado ni kushindwa kumaliza mechi mapema wanapopata nafasi, jambo ambalo linaweza kuwapa Sporting matumaini kama mchezo utaendelea kuwa mgumu. Jisajili na ubeti hapa na Meridianbet mechi hii.
Kwa upande wa Sporting CP, chini ya kocha wa sasa Rui Borges, timu hii imeendelea kuonyesha mpira wa kasi. Lengo lao kubwa katika marudiano haya litakuwa ni kufunga mabao mapema ili kurudisha usawa wa jumla wa matokeo. Sporting watajaribu kuongeza presha ya juu mapema, kujaribu kuvuruga build-up ya Arsenal na kutumia makosa madogo katika ulinzi wao.
Je nani unampa nafasi ya kuondoka na ushindi au kusonga mbele kwenye michuano hii ya Ligi ya Mabingwa kule Ulaya. Suka jamvi lako kwenye mechi hii ya Arsenal dhidi ya Sporting CP.
Mechi nyingine ya kibabe itapigwa kule Allianz Arena Ujerumani ambapo Bayern Munich watawaalika Real Madrid, hii ni mechi ambayo inatarajia kugusa hisia za mashabiki wengi Duniani kutoka na ukubwa wa timu hizi mbiii.
Kwenye mechi ya mkondo wa kwanza kule Santiago Bernabeu Bayern walishinda 2-1 wakiwa wamecheza mchezo mzuri kabisa ambapo kama wangekuwa wametumia nafasi zao vyema basi wangekuwa na uongozi mzuri zaidi.
Bayern Munich wanarejea nyumbani wakiwa na faida ya bao moja, lakini hii nayo haitoshi kwani tumeshuhudia Real akipundua meza haraka sana kwenye michezo kama hii hasa ya kufuzu hatua inayofuta. Kisaikolojia, wanajua kuwa Real Madrid ni timu hatari sana inapokuwa nyuma kwenye matokeo ya aggregate.
Lakini Chini ya kocha Vincent Kompany, Bayern wamekuwa wakijaribu kucheza mpira wa kisasa zaidi umiliki wa mpira, build-up ya taratibu na pressing ya juu. Hata hivyo, tatizo lao linaweza kuwa kujaribu “kulinda faida” badala ya kushambulia, jambo ambalo linaweza kuwapa Madrid nafasi ya kurejea.
Real Madrid ni ni timu yenye “comeback mentality” na tumeshuhudia ikifanya hivyo mara nyingi hata mbele ya Bayern mwaka 2024 walifanya hivyo baada ya Joselu kuingia uwanjani.
Madrid wana DNA ya kushinda mechi kubwa hata wakiwa kwenye wakati mgumu. Hawakimbilii mashambulizi ovyo, bali husubiri muda sahihi wa kuumiza mpinzani kwani wa uzoefu mkubwa wa mechi za hatua ya mtoano, uwezo wa kuvumulia presha ya ugenini na mashambulizi ya moja kwa moja kwani wana wachezaji wenye uwezo wa kufanya hivyo.
Ikumbukwe kuwa hii ni mechi ambayo lolote linaweza kutokea muda wowote kwani timu zote mbili zinaweza kuwa na malengo tofauti, wenyeji wao wanataka kulinda walichonacho lakini kuongeza pia, huku Real wao wakitaka kuweka mzani sawa na ikiwezekana waongoze kwa aggregate. Je wataweza kufanya hivyo?. Bashiri mechi hii leo.


No comments:
Post a Comment