![]() |
| Sehemu ya magari mapya tisa (9) aina ya Toyota Hilux yenye thamani ya shilingi bilioni 1.6 yaliyonunuliwa na TTCL kwa ajili ya kuchochea huduma kwa wateja kwa huduma zake. |
![]() |
| Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Bw. Moremi Marwa akizungumza alipokuwa akikabidhi magari 9 na bajaji 28 ambazo nazo zitatumika kuboresha huduma kimasoko. |
![]() |
| Mkurugenzi wa Ufundi na Uendeshaji TTCL, Eng. Cecil Francis, akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi huo |
SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limenunua magari mapya tisa (9) aina ya Toyota Hilux pamoja na bajaji 28 kwa ajili ya kuchochea utoaji huduma za mawasiliano pamoja na majukumu ya Shirika ikiwemo kuboresha utoaji huduma kwa wateja wake.
Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Bw. Moremi Marwa amekabidi magari hayo leo jijini Dar es Salaam, ambapo alisema Shirika limetumia jumla ya shilingi bilioni 1.6 kununua magari 9 aina ya Toyota Hilux, huku likitumia shilingi milioni 291.2 kununua bajaji 28 ambazo nazo zitatumika kuboresha huduma kimasoko. .
Akizungumza Mkurugenzi huyo alisema TTCL inaendelea na Mpango Mkakati wa Kibiashara wa miaka 10, ambao utekelezaji wake umeanza katika mwaka wa fedha 2025/26, Mpango unaolenga kuleta mageuzi makubwa ndani ya shirika, hususan katika kuimarisha uwajibikaji, kuongeza uzalishaji wenye tija, na kuhakikisha uendelevu wa shughuli zetu.
"Katika mageuzi haya yanayoendelea, mojawapo ya hatua muhimu ni utekelezaji wa mradi wa Faiba - Fiber To The X (FTTx). Mradi huu unalenga kusambaza huduma ya intaneti yenye kasi, uhakika na bora katika makazi, ofisi, na maeneo ya biashara. Kupitia huduma ya “Faiba Mlangoni Kwako,” shirika linaendelea kupanua huduma hizi katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Unguja na mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Dodoma, Mwanza, Geita, Iringa na Mbeya. Aidha, Shirika katika mwaka wa fedha 2026/27 limepanga kufikisha huduma hii ya Faiba katika mikoa iliyobakia nchini.' Alisisitiza Bw. Marwa katika hafla hiyo.
Bw. Marwa, amekabidhi magari tisa (9) na bajaji ishirini na nane (28) kwa Wakuu wa Idara na Vitengo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha utekelezaji wa majukumu ya Shirika na kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja wake.
Hafla hiyo imefanyika Makao Makuu ya Shirika jijini Dar es Salaam, ambapo Mkurugenzi wa Ufundi na Uendeshaji TTCL, Eng. Cecil Francis, Mkurugenzi wa Biashara, Bw. Vedastus Mwita, pamoja na Meneja wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, Bi. Esther Kamulali wakipokea vitendea kazi hivyo vinavyotarajia kurahisisha utoaji wa huduma kwa wateja.
“Uwekezaji huu unaakisi dhamira ya Shirika ya kurejesha faida kwa vitendo kupitia kuimarisha ufanisi wa kazi na utoaji wa huduma. Ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Kibiashara wa miaka 10 unaolenga kuongeza tija, kuimarisha miundombinu na kuboresha huduma kwa wateja,” alibainisha Bw. Marwa akizungumza na wanahabari katika hafla hiyo.
Aidha, alibainisha kuwa vyombo hivyo vitasaidia kwa kiasi kikubwa katika shughuli za kiutendaji ikiwemo usimamizi na matengenezo ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB), utekelezaji wa mradi wa Faiba Mlangoni Kwako, pamoja na shughuli nyingine za kibiashara na kiufundi za Shirika.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Ufundi na Uendeshaji, Eng. Cecil Francis, alimshukuru Mkurugenzi Mkuu kwa uwekezaji huo, akieleza kuwa utarahisisha utendaji kazi wa timu za kiufundi na kuongeza kasi ya utoaji huduma, hususan katika maeneo ya miundombinu









No comments:
Post a Comment